IRGC yapiga ndege nyingine ya kivita ya Marekani aina ya F-18
-
Ndege ya kivita ya F-18
Ndege ya kivita aina ya F-18 ya jeshi la kigaidi la Marekani imepigwa na kutunguliwa kwa kombora la Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kusini mwa nchi.
Idara ya Uhusiano wa Umma ya IRGC imeripoti kwamba operesheni hiyo ilifanywa kwa mafanikio na vitengo vya ulinzi wa anga jana Jumatano.
Ndege ya kivita ya jeshi la Marekani aina ya F-18 ilipigwa ikiwa angani jioni ya jana kwa makombora ya mfumo mpya wa ulinzi wa anga wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, chini ya amri ya mtandao jumuishi wa ulinzi wa anga wa Iran, na kuanguka katika Bahari ya Hindi.
Operesheni hiyo ni ya nne kufanikiwa kutungua ndege za kivita za kimkakati za majeshi ya Marekani na Wazayuni katika anga ya Iran kupitia mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga ambayo imetengenezwa na wataalamu wa Iran. Ndege nyingine tatu za jeshi la Marekani zilitunguliwa zikiwa katika anga ya nchi jirani.
Katika taarifa tofauti mapema Jumatano, IRGC ilisema imetungua ndege isizo na rubani katika anga ya nchi. Ndege hiyo hatari ililengwa na kuharibiwa ikielekea kwenye anga ya kusini mwa Iran.
Idadi ya ndege zisizo na rubani za maadui zilizotunguliwa na ulinzi wa anga wa Iran hadi sasa inafikia karibu ndege 140.
Vikosi vya majeshi ya Iran vimejibu uchokozi wa Marekani na Israel kwa kuvurumisha makombora mengi yanayoongozwa kwa usahihi na ndege zisizo na rubani za kisasa kabisa, na kushambulia ngome na masahi ya Marekani na Israel katika eneo la Magharibi mwa Asia katika mawimbi zaidi ya 80 ya mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyopewa jina la Operesheni Ahadi ya Kweli-4.