Jenerali Mousavi amuonya adui Mzayuni-Mmarekani: Umepiga miundombinu yetu; sasa subiri uone
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137632-jenerali_mousavi_amuonya_adui_mzayuni_mmarekani_umepiga_miundombinu_yetu_sasa_subiri_uone
Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa matamshi ya kujibu mashambulizi ya adui Marekani-Mzayuni dhidi ya miundombinu ya Iran.
(last modified 2026-03-29T00:08:55+00:00 )
Mar 28, 2026 04:32 UTC
  • Jenerali Mousavi amuonya adui Mzayuni-Mmarekani: Umepiga miundombinu yetu; sasa subiri uone

Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa matamshi ya kujibu mashambulizi ya adui Marekani-Mzayuni dhidi ya miundombinu ya Iran.

Brigedia Jenerali Sayyid Majid Mousavi, Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kuhusu mashambulizi ya adui Mzayuni wa Marekani dhidi ya miundombinu ya Iran na kusema: Mlitujaribu mara moja kabla ya hapa; dunia imeona tena namna nyinyi wenyewe mlivyoanza kuchezea moto na kushambulia miundombinu.

Brigedia Jenerali Sayyid Majid Mousavi ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandaoni kwamba: Wakati huu mlinganyo hautakuwa tena wa jicho kwa jicho; Subirini!

Amesema: "Wafanyakazi wa makampuni ya viwanda yenye mfungamano na Wamarekani na utawala wa Kizayuni wanapaswa kuondoka mara moja mahala pa kazi zao, ili kuepusha maisha yao kutumbukia hatarini!"

Wakati huo huo Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, Msemaji Mkuu wa Jeshi la Iran amewataka maadui wajitenge na washauri wao wa Hollywood na kukubali ukweli wa mambo katika medani ya vita.

Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, ameionya Marekani na utawala wa Kizayuni kwa kusema: Iran ina nguvu, na ndio mshindi katika uwanja wa vita, na nchi iliyoshinda ndiyo huweka masharti ya kuhitimisha vita, na bila shaka maadui wa Iran ya Kiislamu watalazimika kuyakubali.

Amesisitiza kwamba: "Mmediriki uwezo wa vikosi vya jeshi na wa taifa kubwa la Iran katika uwanja huo. Hivyo ni bora mjirudi na muache kuota ndoto. Jitengeni na washauri wenu wa Hollywood, na mkubali ukweli wa mambo," amesema Jenerali Shekarchi.