Pezeshkian: Tutailinda Iran kwa azma thabiti na uwezo wetu wote
Rais Mahmoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huku akiashiria kwamba Iran ilishambuliwa kijeshi na Marekani na utawala haramu wa Israel wakati ilipokuwa kwenye mazungumzo na Marekani, amesema: "Sisis tunasisitiza juu ya azma thabiti ya kujilinda."
Katika mazungumzo ya simu na Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan, Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemfahamisha matukio ya hivi karibuni kabisa ya hujuma za kijeshi za Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran pamoja na jinai zao za kivita, yakiwemo mashambulizi dhidi ya shule, hospitali na miundombinu muhimu na ya kiviwanda nchini Iran.
Pezeshkian ameeleza kuwa, Iran ilishambuliwa kijeshi na Marekani na utawala wa Kizayuni wakati ilipokuwa ikifanya mazungumzo na Marekani na kusisitiza azma thabiti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kujilinda kwa kutumia uwezo wake wote.
Katika mazungumzo hayo, Rais wa Azerbaijan pia ameelezea matumaini yake kuwa amani na utulivu vitarejea katika eneo haraka iwezekanavyo, akiashiria matokeo mabaya ya vita dhidi ya amani na uthabiti wa eneo.
Marais wa nchi hizi pia wamebadilishana mawazo kuhusu kuendeleza ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali.