Baghaei: Vita vilivyotwishwa Iran vimelenga utambulisho wa Iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Vita vya kulazimishwa vya Wamarekani na Wazayuni dhidi ya Iran vimelenga uwepo na utambulisho wa Kiirani.
Esmail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameandika ujumbe kwenye mtandao wa X kuhusiana na hujuma za kijeshi za Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuhoji: Je, kushambuliwa shule, vyuo vikuu na hospitali, na tishio la kuirejesha nchi katika zama za mawe, kunaweza kufasiriwa vingine isipokuwa chuki dhidi ya #Iran na #Wairani?!
Ameongeza kwamba kufichuliwa kwa nia mbaya ya adui, ambayo si kingine bali ni chuki ya kidhalili na kihistoria dhidi ya Iran na Wairani, jambo ambalo limekuwa likikaririwa katika matamshi ya watu kama vile Lindsey Graham na Steve Bannon, kwa kutamka maneno kama vile "tofauti ya miaka 2300" au “kurudiwa shambulio la Alexander the Great dhidi ya Iran” na pia viongozi wengine wa Marekani ambao wamekuwa wakitumia maneno ya udhalilishaji kama vile "wendawazimu," "waovu" na “magaidi” kuhusu taifa la Iran na kudai kutaka kulirejesha katika “ zama za mawe”, pamoja na jinai za kutisha na zisizo na mfano wake za adui katika kushambulia shule, hospitali na vituo vya huduma za afya kama vile Taasisi ya Pasteur, vyuo vikuu, maeneo ya kihistoria-kiutamaduni, miundombinu ya uzalishaji bidhaa nchini, ni mambo ambayo yameondoa shaka yoyote kuhusu lengo halisi la vita hivi.
Amesema: ‘Vita hivi vya kulazimishwa vya Marekani na Israel dhidi ya Iran havina lengo jingine isipokuwa kutaka kuangamiza Iran na Wairani. Adui amelenga ujumla, utambulisho, na mizizi ya nchi hii na watu wake, ambapo sote tutaulizwa na kuhukumiwa, mbele ya dhamiri zetu na mbele ya historia, kuhusu mahala na upande wa historia tuliosimama katika siku hizi ngumu na muhimu.’
Baghaei amesisitiza kuwa: Wairani wamethibitisha kwamba wana irada isiyoshindwa ya kutetea ardhi na heshima yao na kuwashinda maadui wavamizi.