Sep 23, 2016 08:17 UTC
  • Qazi-Askari aukosoa Umoja wa Mataifa kwa kunyamazia jinai za Saudia

Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija ameukosoa vikali Umoja wa Mataifa kutokana na kufumbia kwake macho jinai za utawala wa Saudi Arabia.

Hujatul Islam Walmuslimin Sayyid Ali Qazi Askari amesema hayo katika kumbukumbu ya Mashahidi wa Maafa ya Mina na Masjidul Haram iliyofanyika katika mkoa wa Semnan na kuongeza kuwa, licha ya kuwa, Umoja wa Mataifa uliundwa kwa ajili ya kushughulikia matatizo na mizozo, lakini umekubali kunyamazia kimya jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Saud baada ya kupokea pesa.

Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija na Ziara ameashiria baadhi ya mivutano kati ya Tehran na Riyadh na kusisitiza kwamba, utawala wa Aal Saudi unaizushia uwongo Iran kwamba, inaingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine ilihali yenyewe iko kijeshi nchini Yemen na katika nchi nyingine imekuwa ikiwatumia magaidi na mamluki wake wa kitakfiri kufanya mauaji.

Maafa ya Mina

Sayyid Ali Qazi Askari ameongeza kuwa,  falsafa ya ibada ya Hija ni Waislamu kukutana na kubadishana mawazo kuhusiana na matatizo yanayowakabili na kuyatafutia ufumbuzi na kueleza kwamba, kama utawala wa Saudia usingeleta matatizo katika kuendesha ibada ya Hija, basi matatizo yanayoshuhudiwa hii leo katika ulimwengu wa Kiislamu yasingekuwepo.

Tags