Iran yaendelea kustawisha miradi yake ya nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i21172-iran_yaendelea_kustawisha_miradi_yake_ya_nyuklia
Naibu wa Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inaendelea kustawisha miradi yake ya nyuklia kwa malengo ya amani.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Dec 10, 2016 23:38 UTC
  • Iran yaendelea kustawisha miradi yake ya nyuklia

Naibu wa Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inaendelea kustawisha miradi yake ya nyuklia kwa malengo ya amani.

Ali Asghar Zareian alisema hayo jana (Jumamosi) katika sherehe za ufunguzi wa maonyesho ya 36 ya maendeleo ya nyuklia ya Iran katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Shahroud, mashariki mwa Tehran na kuongeza kuwa, uwazi na ustawi uliopo katika miradi ya amani ya nyuklia na katika sekta nyinginezo za kielimu za Iran utaendelea kwa kushirikiana pande zote husika hadi kuifikisha Iran kwenye vilele vya juu ya ustawi wa kielimu.

Zareian amesisitiza kuwa, dola la Marekani limezidi kuwa dhaifu na kuongeza kwamba: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuwa na muono wa mbali na kwa kumtambua vizuri adui imeweza kufungua njia ya ustawi wa kielimu katika nyuga tofauti na leo hii Taasisi ya Nishati ya Atomiki ni nembo ya nguvu za Jamhuri ya Kiislamu.

Baadhi ya pande zilizotia saini makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. Mjumbe wa Russia hayumo pichani

 

Naibu wa Mkuu wa Taasisi ya Nyuklia ya Iran ameashiria pia jinsi upande wa pili wa mazungumzo ya nyuklia usivyoheshimu ahadi zake kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kuwa: Tangu mwanzoni mwa utekelezaji wa makubaliano hayo, kulibuniwa "vifurushi" vya kiutaalamu ili viwe muongozo wa kusimamia utekelezaji huo kutokana na kuhofiwa kuvunjwa JCPOA na baadhi ya nchi hasa Marekani.

Amesema, miongoni mwa matunda ya utekelezaji wa makubaliano hayo ya nyuklia ni kuuziwa Iran tani 230 za keki ya njano ya nyuklia katika mkabala wa kusafirisha nje tani 8.5 za urani iliyorutubishwa.