"Kiongozi Muadhamu katu hatoruhusu vitisho kutoka kwa maadui"
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, katu hatokubali vitisho na chokochoko za maadui.
Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema kuwa, matamshi yalitolewa jana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi wa Kiislamu alipokutana na wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Mkuu wa Iran, ndio suluhuhisho na jibu la changamoto zinazoikabili Iran ya Kiislamu.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, jana asubuhi alikutana na kuzungumza na mkuu pamoja na wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi wa Mapinduzi, ambapo aliashiria hatua na aina tofauti za uadui wa kambi ya mabeberu wa dunia dhidi ya Iran na kubainisha kuwa, mbinyo mkali wa kiuchumi na hujuma kubwa na pana lakini za kimya kimya katika uga wa utamaduni, ni miongoni mwa mihimili mikuu ya upangaji na utekelezaji inayofuatiliwa na kambi ya adui na kuwafanya wananchi wavunjike moyo na Mfumo wa Kiislamu; na kwa njia hiyo kuweza kuiondoa nguzo hiyo kuu inayotegemewa na viongozi ili kuweza kusimama kidete kukabiliana na adui.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amebainisha kuwa, uchumi, maadili, utamaduni na sayansi ndio mambo anayoyapa kipaumbele Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ayatullah Muhammad Emami Kashani, Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa ya hapa mjini Tehran amefafanua kuwa: "Kama alivyoashiria Kiongozi Muadhamu siku ya Alkhamisi, tunaona fahari kwa utamaduni wa Kiirani, Jamhuri ya Kiislamu, utamaduni wa kuwahimiza Wapalestina wasimame kidete mbele ya Wazayuni, kuwatetea wananchi wa Yemen kutokana na jinai dhidi yao zinazofanywa na utawala wa Aal Saud, na kuwapa moyo Wairaqi juu ya kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh; huu ndio utamaduni ambao unawapa mafunzo wanadamu, na unaoleta ufanisi katika jamii."
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa Tehran ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima inayapa uzito mambo yanayouhusu ulimwengu wa Kiislamu.