Jeshi la Iran lafanya mazoezi ya makombora
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i2689-jeshi_la_iran_lafanya_mazoezi_ya_makombora
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran IRGC linafanya awamu ya mwisho ya mazoezo makubwa ya makombora ya kijihami.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 08, 2016 14:58 UTC
  • Jeshi la Iran lafanya mazoezi  ya makombora

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran IRGC linafanya awamu ya mwisho ya mazoezo makubwa ya makombora ya kijihami.

Duru ya mwisho ya mazoezi hayo yaliyopewa jina la Eqtedar-e-Velayat ilihusidha makombora ya balistiki kurushwa kutoka katika maghala maalumu ya chini ya ardhi kote Iran.

Katika taarifa IRGC imesema mazoezi hayo yanalenga kuonyesha uwezo wa Iran kuhijami na kuzuia adui sambamba na kuwa tayari jeshi kukabiliana na vitisho vyote dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu na ardhi ya Iran.

Kamanda Mkuu wa IRGC Meja Jenerali Mohammad Ali Jafari amesema na mkuu wa kitengo cha anga za mbali katika IRGC Brigedia Jenerali Amirali Hajizadeh walisimamia mazoezo hayo.

Mwezi Oktoba mwaka jana Iran ilifanyia majaribio yaliyofana kombora la masafa marefu la balisitiki la Emad lenye uweo wa kulenga shabaha kwa ustadi mkubwa jambo ambalo liliwakera sana wanasiasa wa Marekani.