Qassemi: Marekani inatumia viwango vya undumakuwili katika kupambana na ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i28502-qassemi_marekani_inatumia_viwango_vya_undumakuwili_katika_kupambana_na_ugaidi
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani inatumia viwango vya undumakuwili katika kupambana na ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 01, 2017 09:17 UTC

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani inatumia viwango vya undumakuwili katika kupambana na ugaidi.

Bahram Qassemi amesema hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari wa ndani na nje ambapo akijibu swali kuhusiana na hatua ya Marekani ya kupokea kwa mikono miwili uwepo wa kundi la kigaidi la  Mujahidin Khalq (MKO) huko Albania na himaya na uungaji mkono rasmi wa Washington kwa ugaidi amesema kuwa, uungaji mkono wa Marekani kwa ugaidi si jambo geni kwani limekuwepo tangu huko nyuma na kwamba, Washington inapenda kutumia viwango vyake vya undumakuwili katika kupambana na ugaidi.

Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kwamba, wakati mwingi Wamarekani huwaunga mkono magaidi ambao wanadhamini maslahi yao jambo ambalo mwisho wa siku huwa na madhara kwao wenyewe kama ilivyokuwa kwa makundi ya kigaidi ya Taliban na al-Qaeda.

Bahram Qassemi ameongeza kuwa, Iran kupitia njia za kidiplomasia na kupitia ubalozi wake nchini Albania imezitahadharisha nchi zote ulimwenguni kuhusiana na hatari ya kundi hilo la kigaidi la Mujahidin Khalq na kwamba itaendelea kutoa onyo na indhari kuhusiana na hatari ya kundi hilo.

Qassemi amekanusha pia madai ya kuweko mazungumzo kati ya Iran na Marekani nje ya kadhia ya makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA.