Ansari: Hukumu ya mahakama ya Marekani dhidi ya Iran ni kichekesho
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i3001-ansari_hukumu_ya_mahakama_ya_marekani_dhidi_ya_iran_ni_kichekesho
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa hukumu iliyotolewa na mahakama ya Marekani dhidi ya Iran ni kichekesho, haina maana na inachezea shere vyombo vya mahakama na uadilifu na kuzidisha doa jeusi katika utendaji wa mahakama za Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 13, 2016 22:51 UTC
  • Ansari: Hukumu ya mahakama ya Marekani dhidi ya Iran ni kichekesho

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa hukumu iliyotolewa na mahakama ya Marekani dhidi ya Iran ni kichekesho, haina maana na inachezea shere vyombo vya mahakama na uadilifu na kuzidisha doa jeusi katika utendaji wa mahakama za Marekani.

Hussein Jabiri-Ansari amesema hukumu ya mahakama hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni bidhaa mpya ya mahakama za nchi hiyo katika medani ya ushindani wa kufuata kibubusa sera za Wazayuni za kueneza hofu na chuki dhidi ya Iran. Amesema kuwa hukumu hiyo pia inatoa ujumbe hatari kwa magaidi na waungaji mkono wao na kuwahamasisha kuwaua watu wa Marekani na nchi nyingine duniani.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameongeza kuwa, serikali ya Marekani imeshirikiana na mahaka ya nchi hiyo katika kutoa hukumu kama hiyo.

Itakumbukwa kuwa mahakama moja ya jimbo la New York imetoa hukumu ya kustaajabisha ikidai kuwa Iran inawajibika kulipa dola bilioni 10 na nusu kwa familia za wahanga wa mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 na makampuni ya bima. Hii ni licha ya kwamba watu 15 kati ya 19 waliotekeleza mashambulizi hayo walikuwa raia wa Saudi Arabia, Waimarati wawili, Mlebanon mmoja na Mmisri mmoja na wala hakuwamo raia hata mmoja wa Iran.