Utambulisho wa kweli wa Marekani kwa mtazamo wa Kiongozi Muadhamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i30410-utambulisho_wa_kweli_wa_marekani_kwa_mtazamo_wa_kiongozi_muadhamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya jana alikutana na viongozi wa mihimili mikuu mitatu ya dola, maafisa wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na majimui ya wakurugenzi ambapo katika sehemu ya hotuba yake alibainisha utambulisho halisi wa Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 13, 2017 08:27 UTC

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya jana alikutana na viongozi wa mihimili mikuu mitatu ya dola, maafisa wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na majimui ya wakurugenzi ambapo katika sehemu ya hotuba yake alibainisha utambulisho halisi wa Marekani.

Ayatullah Ali Khamenei ameashiria hatua chafu zilizochukuliwa na Wamarekani baada ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, nguvu za kibeberu zimekuwa zikitumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kutwisha matakwa yake ambapo moja ya mikakati hiyo ni ile iliyopewa jina la "vigezo na kanuni za kimataifa" ili kupitia njia hiyo wazituhumu nchi zinazojitawala na zinazopinga dhulma kuwa zinakiuka vigezo na kanuni za kimataifa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbusha matamshi ya hivi karibuni ya Wamarekani kwamba, katika matamshi yao ya kipropaganda wanalizungumzia suala la kupandikiza ukosefu wa amani katika Mashariki ya Kati kama ni "vigezo na kanuni za kimataifa."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akiwahutubia viongozi wa mihimili mikuu mitatu ya dola, maafisa wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na majimui ya wakurugenzi

Kwa hakika matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kufichua na kuweka wazi malengo ya Marekani ya kutumia "vigezo na kanuni za kimataifa" ambapo kama hilo litafikiriwa kwa njia sahihi, basi chimbuko la matatizo mengi litafahamika. 

Noam Chomsky, mwanasiasa na mwananadharia mashuhuri wa Kimarekani, hivi karibuni alisema alipokuwa akijibu swali kuhusiana na matamshi ya viongozi wa Marekani kwamba, Iran ndio tishio kubwa kuwa: Marekani inaiona Iran kuwa ni tishio kubwa kwa ajili ya amani, lakini kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika ndani ya Marekani kwenyewe na uchunguzi wa maoni wa shirika la Galup ni kuwa, walimwengu wanaamini kwamba, Marekani ndio tishio kubwa zaidi kwa ajili ya amani ya dunia.

Hata hivyo Chomsky sio mtu pekee ambaye amekuwa akizungumzia ukweli kuhusiana na utambulisho halisi wa malengo ya siri na ya dhahiri ya Marekani katika uwanja huu. Kuhusiana na ukweli huu huu, Rand Paul seneta wa chama cha Republicans miezi michache iliyopita alisema: Tumekuwa na wasiwasi na Iran kiasi kwamba, tumesahau nafasi ya kuchupa mipaka ya Mawahabi wa Saudi Arabia katika machafuko ya Mashariki ya Kati na vilevile ugaidi wa kimataifa. Rand Paul alibainisha kwamba, sehemu kubwa ya uungaji mkono kwa misimamo ya uchupaji mipaka na ugaidi ni kutoka Saudia na sio Iran. 

Marekani ina nafasi na mchango mkubwa katika kuibuka vita na mivutano  ya kimataifa sambamba na ukiukaji wa mikataba ya kimataifa kuanzia mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Tokyo Japan, maafikiano ya Paris Ufaransa bila kusahau upuuuzaji wa Washington kwa mkataba wa kuzuia uzalishaji na usambazaji wa silaha za nyuklia NPT na kutumia silaha za nyuklia hadi kuanzisha vita kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Aidha Marekani imekuwa kikwazo cha biashara huru ulimwenguni huku ikiyaunga mkono makundi ya kigaidi kama Daesh ambapo kila moja kati ya hayo ni mfano wa wazi wa ukiukaji wa kanuni za kimataifa unaofanywa na serikali ya Marekani,

Noam Chomsky, mwananadharia wa Kimarekani

Kwa hakika hatua hizi za uharibifu za Marekani zinatosha kuwafanya walimwengu wafahamu utambulisho halisi wa Washington kieneo na kimataifa.

Hapana shaka kuwa nukta zilizosisitizwa na kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alasiri ya jana mbele ya viongozi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kuhusiana na masuala mbalimbali zina umuhimu wa pande kadhaa ambapo kufahamu na kuzingatia utambulisho wa kweli wa Marekani kunahesabiwa kuwa mojawapo ya pande hizo. Hata hivyo sehemu nyingine na muhimu zaidi ni stratejia na mikakati mikubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na vitisho, miamala na njama za Marekani dhidi ya taifa hili katika uga wa kimataifa.

Kiongozi Muadhamu amesema bayana kwamba, masuala kama haki za binadamu, ugaidi na madai kwamba, Iran inavuruga usalama wa Mashariki ya Kati ni visingizio tu vya Marekani dhidi ya Mfumo wa Kiislamu na kubainisha kwamba, Marekani yenyewe ndio gaidi na mlezi wa magaidi na imekuwa ikiunga mkono tawala kama Israel ambayo ni ubongo wa ugaidi na ilijitokeza toka siku ya kwanza kwa dhulma na mauaji.