Pongezi za Waziri wa Ulinzi wa Iran kufuatia kukombolewa mji wa Mosul
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i31562-pongezi_za_waziri_wa_ulinzi_wa_iran_kufuatia_kukombolewa_mji_wa_mosul
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe akiwapongeza Waziri wa Ulinzi na Kamanda wa harakati ya kujitolewa ya wananchi wa Iraq kwa jina la Hashdu Sha'abi kufuatia ushindi wa jeshi na vikosi hivyo vya wananchi katika kuukomboa kikamilifu mji wa Mosul.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 09, 2017 23:28 UTC
  • Pongezi za Waziri wa Ulinzi wa Iran  kufuatia kukombolewa mji wa Mosul

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe akiwapongeza Waziri wa Ulinzi na Kamanda wa harakati ya kujitolewa ya wananchi wa Iraq kwa jina la Hashdu Sha'abi kufuatia ushindi wa jeshi na vikosi hivyo vya wananchi katika kuukomboa kikamilifu mji wa Mosul.

Haidar al Abadi Waziri Mkuu wa Iraq jana Jumapili alielekea katika mji wa Mosul kaskazini mwa mji mkuu Baghdad na kutangaza rasmi ushindi wa jeshi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh baada ya kukaliwa kwa miezi 37. Oparesheni ya kuukomboa mji wa Mosul ilianza tangu Oktoba 17 mwaka jana. 

Brigedia Jenerali Hussein Dehqan  Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumapili alituma jumbe tofauti kwa Mahmoud Abdulghafour Abdallah al Hayali Waziri wa Ulinzi na Hadi al Aamri Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq na kueleza kuwa ni vigumu kuusambatisha ugaidi bila ya kuwepo irada ya kweli na kushirikiana serikali mbalimbali sambamba na kuasisiwa harakati moja dhidi ya ugaidi; na kwamba ushindi mkubwa uliopatikana huko Mosul umepelekea kuzimwa njama za Marekani na utawala ghasibu wa Kizayuni huko Iraq. 

Vikoso vya kjitolea vya wananchi wa Iraq katika mapambano dhidi ya Daesh

Brigedia Jenerali Dahqan amesema anataraji kuwa stratejia ya vita vya niaba vya mfumo wa uistikbari katika eneo la Mashariki ya Kati itagonga mwamba na kwamba, ushindi uliopatikana hivi sasa huko Iraq ni natija ya kuwa na ikhlasi na kujitolea vikosi vya Hashdu Sha'abi chini ya uongozi wa busara wa Marjaa mkuu wa Kishia na makamanda shupavu wa Iraq.  Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema Tehran iko tayari kikamilifu kuimarisha na kustawisha ushirikiano wa kiulinzi, kijeshi na kiusalama kati yake na Iraq.