Brigedia Jenerali Jazayeri: Marekani inapaswa kupewa somo jipya
Msemaji wa majeshi ya Iran amelaani vitisho na madai yanayotolewa na Rais Doland Trump wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, umewadia wakati wa kutolewa somo jipya kwa Marekani.
Brigadia Jenerali Massoud Jazayeri amesema inaonekana kuwa serikali ya Donald Trump haielewi chochote isipokuwa matusi na inahitaji kushituliwa ili ijifunze dhana mpya ya nguvu katika ulimwengu wa leo.
Msemaji wa majeshi ya Iran amesema kuwa, kukabiliana na uchokozi wa Marekani ni jambo muhimu na lililofanyiwa mazoezi na kuongeza kuwa: "Kipindi cha kuwepo kibabe kwa Marekani katika eneo la magharibi mwa Asia kimefikia ukomo na fikra ya Kimarekani ya kuanzisha Mashariki ya Kati Mpya imekwisha kufa. Amesema kuwa mienendo ya Marekani inawasumbua na kuwakera walimwengu na umefika wakatti wa kutoa somo jipya kwa serikali ya Washington.
Meja Jenerali Jazayeri amesisitiza kuwa, uwezo wa kujihami wa Iran hauwezi kamwe kuyumbishwa na bwabwaja za madola ya kigeni na kusema: "Sera na mantiki ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran ya kuongeza nguvu ya kujihami ya nchi ni suala lisilo na shaka."
Ameongeza kuwa Iran imezingatia mipango kabambe ya kukabiliana na sera za kiadui za Marekani.