Ayatullah Shahroudi: Kushindwa Daesh(ISIS) kutausukuma ubeberu uanzishe njama mpya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i36801-ayatullah_shahroudi_kushindwa_daesh(isis)_kutausukuma_ubeberu_uanzishe_njama_mpya
Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa kuwa macho na njama za ubeberu wa kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 26, 2017 00:13 UTC
  • Ayatullah Shahroudi: Kushindwa Daesh(ISIS) kutausukuma ubeberu uanzishe njama mpya

Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa kuwa macho na njama za ubeberu wa kimataifa.

Ayatullah Sayyid Mahmoud Hashemi Shahroudi amesema kuwa, kushindwa na kusambaratishwa kundi la kigaidi la Daesh kutausukuma ubeberu upange na kuanzisha njama mpya.

Ayatullah Shahroudi amesema hayo katika kikao cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  ambapo sambamba na kutoa mkono wa kheri na pongezi kwa kambi ya muqawama na mapambano mkabala na kundi la kigaidi la Daesh huko Iraq na Syria amebainisha kwamba, wananchi na serikali za Iraq na Syria hazipaswi kughafilika na njama za Marekani na utawala haramu wa Israel.

Wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh

Ameongeza kuwa, licha ya kuwa kambi ya muqawama itaibuka mshindi na kuzishinda njama za maadui, lakini wananchi pamoja na serikali za Syria na Iraq hazipaswi kughafilika hata kidogo na njama za Marekani na Israel.

Ikumbukwe kuwa, Jumanne iliyopita, Meja Jenerali Qassem Suleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alimtumia ujumbe Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akitangaza kuangamizwa satwa ya kundi khabithi na la kigaidi la Daesh.