Araqchi: Hatua yoyote ya kuvuruga mapatano ya JCPOA itakuwa na mwisho mbaya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i42238
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita za kundi la 5+1 ni mapatano ya kiusalama na yanahusiana moja kwa moja na usalama wa eneo la Mashariki ya Kati na wa kimataifa, na uvurugaji wa aina yoyote wa makubaliano hayo utakuwa na matokeo mabaya kwa jamii ya kimataifa.
(last modified 2025-07-20T14:05:14+00:00 )
Mar 26, 2018 15:12 UTC
  • Araqchi: Hatua yoyote ya kuvuruga mapatano ya JCPOA itakuwa na mwisho mbaya

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita za kundi la 5+1 ni mapatano ya kiusalama na yanahusiana moja kwa moja na usalama wa eneo la Mashariki ya Kati na wa kimataifa, na uvurugaji wa aina yoyote wa makubaliano hayo utakuwa na matokeo mabaya kwa jamii ya kimataifa.

Abbas Araqchi amesema kuwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa ambapo Rais Donald Trump wa Marekani anafanya njama za kuvuruga makubaliano hayo ya nyuklia au kutoa wito wa kufanyiwa mabadiliko lakini amefeli na kushindwa. 

Araqchi amesema kuwa, jamii ya kimataifa na hata waitifaki wa Ulaya wa Marekani wanapinga matakwa hayo ya Donald Trump na vilevile azimio la Baraza la Usalama lililoidhinisha makubaliano hayo ya JCPOA linapingana na matakwa ya Marekani. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema hatua yoyote ya kujiondoa Marekani katika makubaliano hayo pia itakuwa na matokeo machungu sana kwa nchi za Magharibi, Marekani na Ulaya na kuharibu kabisa hadhi ya nchi hiyo kote duniani. 

Donald Trump

Abbas Araqchi amesisitiza kuwa, kama alivyosema Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Bi Federica Mogherini, JCPOA ni makubaliano ya kiusalama yanayohusiana moja kwa moja na usalama na amani ya kimataifa na kuvugwa kwake kutakuwa na matokeo mabaya kwa jamii yote ya kimataifa.

Araqchi amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejitayarisha kwa ajili ya machaguo yote na itatoa jibu kwa hatua yoyote itakayochukuliwa na Trump na wengineo dhidi ya makubaliano hayo ya nyuklia.