Larijani: Marekani imedhamiria kuifuta taasisi ya Umoja wa Mataifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i44506-larijani_marekani_imedhamiria_kuifuta_taasisi_ya_umoja_wa_mataifa
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: Marekani imekusudia kuifuta taasisi ya Umoja wa Mataifa ambayo imeundwa kwa madhumuini ya kuleta amani duniani na hivyo kuutumbukiza uga wa kimataifa kwenye machafuko na mchafukoge wa kiusalama.
(last modified 2026-08-12T14:02:06+00:00 )
May 15, 2018 03:29 UTC
  • Larijani: Marekani imedhamiria kuifuta taasisi ya Umoja wa Mataifa

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: Marekani imekusudia kuifuta taasisi ya Umoja wa Mataifa ambayo imeundwa kwa madhumuini ya kuleta amani duniani na hivyo kuutumbukiza uga wa kimataifa kwenye machafuko na mchafukoge wa kiusalama.

Ali Larijani ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa kikao cha kawaida cha bunge. Ameashiria kuhamishiwa Quds ubalozi wa Marekani uliokuweko Tel Aviv licha ya hatua hiyo kulaaniwa na nchi zote duniani na kukinzana na maazimio ya Baraza la Usalama na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kwamba: Marekani ilishachukua uamuzi tangu miaka kadhaa nyuma ya kuifanya taasisi hiyo ya kimataifa isiwe na thamani wala itibari.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha amesema kujitoa Marekani kwenye mkataba wa Paris wa Tabianchi kumekinzana na makubaliano ya Umoja wa Mataifa na kuivamia Iraq pia kulifanywa bila ya kupitishwa na kuidhinishwa na Baraza la Usalama lakini kwa msaada wa waitifaki wake, Marekani iliishambulia na kuivamia kijeshi nchi hiyo; hata hivyo baada ya muda wakalazimika kuondoka Iraq.

Dakta Larijani ameashiria pia jinai iliyofanywa jana utawala wa Kizayuni ya kuwaua wananchi wasio na ulinzi wa Palestina na kuongeza kuwa: jinai hiyo ni doa kubwa la fedhedha kwa utawala wa Kizayuni na Marekani na litabakia katika historia.../