Ayatullah Jannati: Uhai wa Israel umeshafikia ukingoni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i45446-ayatullah_jannati_uhai_wa_israel_umeshafikia_ukingoni
Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kusisitiza kuwa: Uhai wa utawala wa Israel umefikia ukingoni, na muda si mrefu tutasherehekea kuangamizwa kwa utawala huo ili kuifuta shari yake katika kibla cha kwanza cha Waislamu.
(last modified 2026-02-22T09:20:04+00:00 )
Jun 05, 2018 13:51 UTC
  • Ayatullah Jannati: Uhai wa Israel umeshafikia ukingoni

Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kusisitiza kuwa: Uhai wa utawala wa Israel umefikia ukingoni, na muda si mrefu tutasherehekea kuangamizwa kwa utawala huo ili kuifuta shari yake katika kibla cha kwanza cha Waislamu.

Ayatullah Ahmad Jannati amekumbusha kuwa kushiriki kwenye maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ni jukumu la Waislamu wote na kubainisha kwamba wananchi madhulumu wa Palestina wanafarijika kwa kushiriki Waislamu na watetezi wa uhuru kote duniani katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

Ayatullah Jannati amesema, Palestina ni sehemu ya mwili wa Uislamu na kibla cha kwanza cha Waislamu na akaongeza kuwa: Suala la Quds ni suala la Uislamu na Utu na limo kwenye fitra na maumbile ya mwanadamu kwamba inapasa kumtetea na kumhami anayedhulumiwa.

Siku ya Kimataifa ya Quds inaadhimishwa na watetezi wote wa uhuru duniani

Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imetangazwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini (MA) kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds ili Waislamu kote duniani waonyeshe na kutangaza hasira na ghadhabu zao kwa sera za ubaguzi wa rangi za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu yatafanyika hapa nchini Iran na katika nchi zingine duniani Ijumaa ya tarehe 8 Juni itakayosadifiana na tarehe 23 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.../