Shamkhani: Baadhi ya pande Mashariki ya Kati zinajaribu kuitishwa Iraq ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i46320-shamkhani_baadhi_ya_pande_mashariki_ya_kati_zinajaribu_kuitishwa_iraq_ugaidi
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameashiria jitihada za Marekani za kuwaunga mkono masalia ya magaidi katika eneo hili na kueleza kuwa baadhi ya nchi katika eneo hili zinafanya kila ziwezalo kuyumbisha amani na kuitishwa Iraq ugaidi. 
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 25, 2018 23:50 UTC
  • Shamkhani: Baadhi ya pande Mashariki ya Kati zinajaribu kuitishwa Iraq ugaidi

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameashiria jitihada za Marekani za kuwaunga mkono masalia ya magaidi katika eneo hili na kueleza kuwa baadhi ya nchi katika eneo hili zinafanya kila ziwezalo kuyumbisha amani na kuitishwa Iraq ugaidi. 

Ali Shamkhani jana Jumataatu alikuwa na mazungumzo hapa Tehran na Faleh Fayyaz Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Waziri Mku wa Iraq na akaashiria shambulio la Marekani dhidi ya vikosi vya ulinzi vya Iraq na Syria kwa ajili ya kuunga mkono ugaidi. Shamkhani aidha aliongeza kuwa nchi ambazo kwa kuiamini Marekani zinaweza kujidhaminia usalama wao wa ndani na uthabiti katika eneo zinasaidia kuimarika ugaidi.

Katika mazungumzo hayo, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa wa Iran alieleza kusikitishwa na miamala ya baadhi ya nchi za eneo hili ambazo zimegeuka na kuwa washirika wa kiistratijia wa utawala wa Israel na kubainisha kuwa: Serikali zisizo na tajiriba za nchi hizo zinatekeleza hatua za kimaonyesho na za dhihaka lengo likiwa kuficha matatizo yao ya kiuchumi, kiusalama, na kiusalama.  

Katika mazungumzo hayo na Ali Shamkhani, Faleh Fayyaz Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Waziri Mkuu wa Iraq pia ameshukuru uungaji mkono usio na masharti wa serikali, wananchi na vikosi vya ulinzi vya Iran kwa Iraq katika kupambana na ugaidi na kusisitiza kuhusu nafasi muhimu ya Iran katika ushndi wa jeshi la Iraq mbele ya ugaidi.