Jul 06, 2018 13:18 UTC
  • Ayatullah Kashani: Wazayuni wanachochea malumbano baina ya Waislamu wa Kishia na Kisunni

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema kuwa Wazayuni wanaibua hitilafu baina ya Waislamu na katika upande wa pili vyombo vya habari vinashabikia hitilafu hizo ili kuonyesha taswira isiyo sahihi ya Uislamu.

Ayatullah Mohammad Imami Kashani, Khatibu wa Swala ya Ijumaa wiki jii mjini Tehran amesema kuna haja ya kuwepo ukuruba baina ya Waislamu ili adui asiweze kupenya. Ameongeza kuwa, mrengo wa Mashia wenye makao yao Uingereza ambao wanaendesha idadi kadhaa ya vituo vya televisheni kwa njia ya satalaiti ndio wenye kuchochea malumbano baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni na hilo ndilo wanalotaka Wazayuni.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema Utawala wa Faqihi katika zama za ghaiba ya Imamu wa Zama (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake-ATF) ni kigezo cha umoja wa jamii ya Kiislamu. Kwingineko katika hotuba yake, Ayatullah Kashani amesema adui hivi sasa anatekeleza mkakati muhimu wa vita vya kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa pia ametuma salamu za rambi rambi kwa munasaba wa kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Sadiq AS, Imamu wa Sita wa Mdhehebu ya Shia na kusema: "Kama ambavyo katika zama zake Imam Sadiq AS alifuatilia sana suala la kuleta umoja miongoni mwa Waislamu, leo hii pia umoja wa kauli katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni takwa la Imamu wa Zama (ATF)

Jumatatu tisa Julai mwaka 2018 sawa na 25 Shawwal 1439 Hijria Qamaria itasadifiana na kumbukumbua ya kuuawa shahidi Imam Jaafar Sadiq AS.

Tags