Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza awasili Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49611-waziri_wa_mambo_ya_nje_wa_uingereza_awasili_tehran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amewasili Tehran kwa ajili ya mazungumzo na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Iran na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa nchi hii huku akiongoza ujumbe wa kisiasa wa nchi yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 19, 2018 04:12 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza awasili Tehran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amewasili Tehran kwa ajili ya mazungumzo na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Iran na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa nchi hii huku akiongoza ujumbe wa kisiasa wa nchi yake.

Jeremy Hunt mbali na kufanya mazungumzo na Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje, atakuwa na mazungumzo pia na Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran. Uhusiano wa pande mbili, matukio ya kieneo na kimataifa na Makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ni miongoni mwa masuala ambayo yatajadiliwa katika ziara hii ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza mjini Tehran. 

Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambaye atakuwa mwenyeji wa Jeremy Hunt

Hii ni safari ya kwanza kufanywa na Jeremy Hunt hapa Tehran baada ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza. Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza hapa Tehran inafanyika baada ya kutekelezwa duru ya pili ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na inaonekana kuwa suala la mfumo maalumu wa miamala ya kifedha (SPV) uliopendekezwa na Ulaya kwa ajili ya kudhamini maslahi ya Iran katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na hatua nyingine za Ulaya katika uwanja huo ni kati ya mambo ambayo huenda yakajadiliwa na kuchunguzwa katika ziara hii ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza mjini Tehran.