Feb 09, 2019 17:17 UTC
  • Waislamu wakumbuka kufa shahidi kwa Bibi Fatima al Zahra (as)

Mamilioni ya Waislamu nchini Iran na nchi nyingine kadhaa duniani leo wameshiriki katika vikao na majlisi za kukumbuka siku ya kufa shahidi binti kipenzi wa Mtume wetu Muhammad (saw), Bibi Fatumatu Zahra (as).

Vikao, majlisi na shughuli ya kukumbuka siku ya kufa shahidi Bibi Fatima (as) zilifanyika katika misikiti, husseiniya, kumbi na maeneo ya umma katika miji mbalimbali ya Iran ambako wanazuoni na wasomi wa Kiislamu wamehutubia vikao hivyo na kutaja sifa na matukufu ya binti huyo wa Mtume wetu Muhammad (saw).

Mjini Tehran shughuli kubwa zaidi ya kuomboleza tukio la kufa shahidi BiBi Fatima (as) ilifanyika katika Medani ya Fatimi ambako wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) walikusanyika na kutegea sikio hotuba za wazungumzaji waliosimulia masaibu yaliyompata Bibi Fatima (as) hususan baada ya kufariki dunia baba yake kipenzi, Mtume Muhammad (saw). 

Waislamu wakikumbuka kufa shahidi kwa Bibi Fatima (as)

Bibi Fatima alikuwa na nafasi kubwa na alitoa mchango wa aina yake katika jamii ya Kiislamu. Alikuwa dhihirisho la uchamungu, ukarimu, kujitolea, subira, kujipinda katika ibada na kuwasaidia watu wote na alilea watu adhimu kama Imam Hassan, Hussein na Bibi Zaina (as). Bibi huyo mwema ambaye Mtume (saw) anasema kuwa ni mbora wa wanawake duniani, alikufa shahidi tarehe 3 Jumadithani miezi kadhaa tu baada ya kuaga dunia baba yake, Mtume wa Uislamu, Muhammad (saw). 

Tags