Aug 07, 2022 03:01 UTC
  • Kiongozi Muadhamu ashiriki katika maombolezo ya Tasua ya Imam Husain AS

Usiku wa kuamkia leo umesadifiana na usiku wa mwezi tisa Mfunguo Nne, Muharram, siku ambayo ni maarufu kwa jina la Tasua ya Imam Husain AS.

Maombolezo ya usiku wa kuamkia leo yamefanyika katika kona zote za Iran na nje ya Iran ikiwemo Husainia ya Imam Khomeini MA hapa mjini Tehran na kuhudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Katika kumbukumbu hizo za mapambano ya Aba Abdillahil Husain AS ya mwaka 61 Hijria katika jangwa la Karbala la Iraq ya hivi sasa, kumetolewa khutba kuhusu wajibu wa kuilinda dini ya Allah ya Uislamu kwa moyo mkunjufu na ikhlasi kamili na kutambulisha mapambano ya Imam Husain AS huko Karbala kwa njia za kimantiki na kwa moyo mmoja.

Hujjatul Islam Walmuslimin Masoud Ali katika khutba ya usiku wa kuamkia leo, siku ya Tasua ya Imam Husain AS

 

Katika khutba yake kwenye maombolezo hayo, Hujjatul Islam Walmuslimin Masoud Ali amesema kuwa, leo hii uendelezaji wa kivitendo wa mapambano hayo ya Karbala ni kuoneshwa hasira za walimwengu dhidi ya dhulma za maadui wa Ahlul Bayt wa Mtume SAW, kusimama imara mataifa ya dunia kupambana na madola ya kibeberu na kitaghuti na kuzuia kuenea tamaduni chafu za maadui wa Mwenyezi Mungu katika jamii za Waislamu.

Katika kumbukumbu hizo, Bw,. Mahdi Rasuli amesoma mashairi ya kuomboleza maafa waliyobebeshwa watu kutoka kizazi cha Bwana Mtume Muhammad SAW katika jangwa la Karbala mwaka huo wa 61 wa Hijria.

Tags