Zarif: Kinyume na Saudia, Iran haitaki mvutano na upande wowote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i52087-zarif_kinyume_na_saudia_iran_haitaki_mvutano_na_upande_wowote
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran haitaki kuwa na mvutano na nchi yoyote ile ikiwemo Saudi Arabia.
(last modified 2026-02-22T02:21:18+00:00 )
Mar 11, 2019 03:13 UTC
  • Zarif: Kinyume na Saudia, Iran haitaki mvutano na upande wowote

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran haitaki kuwa na mvutano na nchi yoyote ile ikiwemo Saudi Arabia.

Muhammad Javad Zarif aliyasema hayo jana jioni katika mkutano na waandishi wa habari mjiini Baghdad. Kuhusu uwezekano wa kufanya safari huko Riyadh, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kwamba hana mpango wa kwenda Saudi Arabia lakini hakuna tatizo lolote la kuchukua hatua kama hiyo kwa sababu Iran haitaki kuwa na mivutano na serikali ya Riyadh, na ni Wasaudia ndio waliowasha moto wa ghasia na machafuko katika eneo hili la magharibi mwa Asia. 

Muhammad Javad Zarif pia ameilaumu Marekani kwa kukiuka sheria na kusema: Washington haitosheki na kuvunja sheria bali imekuwa ikizilazimisha nchi nyingine kukanyaga sheria za kimataifa.

Zarif akizungumza na waandishi wa habari, Baghdad

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ametaja sera ya Marekani ya kukiuka sheria za kimataifa na kuziadhibu nchi nyingine kwa sababu tu ya kushikamana kwao na sheria hizo kuwa ni "hatari kubwa".

Zarif amesema anatarajia kuwa, nchi zote duniani zitasimama kidete kukabiliana na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani kama ilivyofanya Iraq na Umoja wa Ulaya.