Zarif: Quds haiuzwi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i53806-zarif_quds_haiuzwi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Quds haiuzwi na ni kibla cha kwanza cha Waislamu na kituo cha matarajio ya Waislamu wote.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 30, 2019 08:11 UTC
  • Zarif: Quds haiuzwi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Quds haiuzwi na ni kibla cha kwanza cha Waislamu na kituo cha matarajio ya Waislamu wote.

Akizungumza jana usiku katika karamu ya futari iliyoandaliwa mabalozi wa nchi za Kiislamu hapa Tehran, Muhammad Javad Zarif amebainisha kuwa Ulimwengu wa Kiislamu unakabiliwa na hali ya kusikitisha hivi sasa; na kwamba hakuna huzuni na hatari kubwa zaidi kuona baadhi ya nchi za eneo zinaunga mkono mpango wenye kufedhehesha wa Muamala wa Karne.

"Muamala wa Karne" ni mpango mpya uliopendekezwa na Marekani kwa lengo la kufutilia mbali na kukandamiza haki za wananchi wa Palestina. Mpango huo umeandaliwa kwa kushirikiana na kufikiwa mapatano baina ya Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia. Kwa mujibu wa mpango huo, Quds Tukufu itakabidhiwa utawala wa Kizayuni; wakimbizi wa Kipalestina walioko nje ya nchi hawatakuwa na haki ya kurejea Palestina' Palestina itamiliki tu ardhi zitakasozalia katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza. 

Katika fremu ya mpango huo wa hila wa "Muamala wa Karne"; Rais Donald Trump wa Marekani Disemba Sita mwaka 2017 aliutangaza mji wa quds unaokaliwa kwa mabavu kuwa mji mkuu wa utawala bandia wa Israel na akatangaza pia uamuzi wake wa kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Quds. Serikali ya Marekani tarehe 14 mwezi Mei mwaka jana ilitekeleza kivitendo uamuzi wake huo. Mji wa Quds unakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni tangu mwaka 1967.  

Uzinduzi wa ubalozi wa Marekani katika mji wa Quds