Rouhani: Shahidi Soleimani alisambaratisha njama za Wazayuni na Marekani katika eneo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i69538-rouhani_shahidi_soleimani_alisambaratisha_njama_za_wazayuni_na_marekani_katika_eneo
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alisambaratisha njama za Wazayuni na Marekani katika eneo na alikuwa mshauri bora zaidi katika sera za kigeni katika eneo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 28, 2021 07:45 UTC
  • Rouhani: Shahidi Soleimani alisambaratisha njama za Wazayuni na Marekani katika eneo

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alisambaratisha njama za Wazayuni na Marekani katika eneo na alikuwa mshauri bora zaidi katika sera za kigeni katika eneo.

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo leo katika kikao cha baraza la mawaziri mjini Tehran na kuongeza kuwa hivi sasa ni wakati wa kukasirika utawala wa Israel, tawala zinazopinga mabadiliko katika eneo na wenye misimamo ya kufurutu ada nchini Marekani.  Rais wa Iran ameongeza kuwa, mkondo waliokuwa wameuchukua umevurugika na kuongeza kuwa: "Trump ni rais pekee wa Marekani ambaye alikuwa mamluki wa Wazayuni. Tab'an marais wengine wa Marekani walikuwa wakishirikiana na kuwaunga mkono Wazayuni lakini hawakuwa mamluki."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameendelea kusema kuwa, Wazayuni ndio waliomchochea Trump ajiondoe katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Aidha amesema kitendo cha kuhamisha mji mkuu wa utawala bandia wa Israel kutoka Tel Aviv hadi Quds (Jerusalem) ni jinai nyingine ya Wazayuni na kuongeza kuwa, hatua ya Trump ya kujiondoa katika baadhi ya mashirika ya kimataifa kwa kisingizio cha Palestina pia nayo ilitekelezwa kwa amri ya Wazayuni.

Rais Rouhani ameongeza kuwa, shahidi Luteni Kanali Soleimani aliuawa kigaidi kwa uchochezi wa Wazayuni na kuongeza kuwa: "Ni kweli kuwa, muuaji alikuwa ni Trump lakini Wazayuni ndio waliokuwa nyuma ya  pazia ya mauaji ya kigaidi ya jenerali huyo mkubwa ambaye alitoa maisha yake muhanga kwa maslahi ya amani katika eneo."

Rais wa Iran amesema leo wenye hasira ni utawala wa Kizayuni, tawala zinazopinga mabadiliko katika eneo na Marekani na hasira hizo zinatokana na mafanikio ya taifa la Iran. Rais Rouhani ameongeza kuwa: "Leo wana hasira kwa sababu njama zote walizozipanga kwa muda wa miaka minne zimesambaatika na sasa nchi zote za kundi la 4+1, ikiwemo Marekani yenyewe, zinafahamu kuwa,  hazina budi ila kusalimu amri mbele ya sheria, kanuni za kimataifa na mantiki ya Iran."