Iran imeuza bidhaa zake za nano katika zaidi ya nchi 45
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i69676-iran_imeuza_bidhaa_zake_za_nano_katika_zaidi_ya_nchi_45
Katibu wa Idara ya Taifa ya Ustawi wa Teknolojia ya Nano nchini Iran amesema hivi sasa bidhaa za teknolojia hiyo zilizotengenezwa Iran zinauzwa katika zaidi ya nchi 45 duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 02, 2021 03:23 UTC
  • Iran imeuza bidhaa zake za nano katika zaidi ya nchi 45

Katibu wa Idara ya Taifa ya Ustawi wa Teknolojia ya Nano nchini Iran amesema hivi sasa bidhaa za teknolojia hiyo zilizotengenezwa Iran zinauzwa katika zaidi ya nchi 45 duniani.

Saeed Sarkar Katibu wa Idara ya Kitaifa ya Ustawi wa Teknolojia ya Nano nchini Iran  amesema bidhaa za Iran za teknolojia ya nano zimeuzwa katika nchi kama Australia, Korea Kusini, China, bara Ulaya na Amerika ya Latini.

Amesema teknolojia mpya kama teknolojia ya nano ni muhimu sana duniani, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kupata nafasi muhimu katika teknolojia hiyo.

Sarkar amesema Iran imenufaika na teknolojia ya nano katika sekta 18 za viwanda na hivi karibuni pia bidhaa mpya zitazalishwa katika uga huo.

Satalaiti ya Iran iliyotegenezwa kwa kutumia teknolojia ya nano

Amesema kwa mafanikio ambayo Iran imepata, si tu kuwa itaweza kukidhi mahitaji yake bali pia itakidhi mahitaji ya nchi zingine duniani.

Miaka 42 baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kati ya mafanikio makubwa ambayo yameweza kupatikana ni ustawi wa kasi katika uga wa sayansi na teknolojia.

Iran inahesabiwa kuwa miongoni mwa nchi 10 bora duniani katika uga wa teknolojia ya nano.