Mkuu wa IRIB Kimataifa alipongeza Shirika la Habari la Iran Press
Sambamba na tarehe 8 Agosti ambayo ni Siku ya Kitaifa ya Wanahabari nchini, Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB, Dkt. Peyman Jebelli alitembelea Shirika la Habari la Iran Press na kusema juhudi na bidii ni ufunguo wa mafanikio makubwa ya shirika hilo.
Dkta Jebelli, ametembelea ofisi ya Shirika la Habari la Iran Press, ambalo ni sehemu ya Kitengo cha Kimataifa cha IRIB ambapo amewapongeza wafanyikazi wa shirika hilo kutokana na jitihada zao.
Jebelli amesema: "Shirika la Habari la Iran Press katika kipindi kifupi na muundo mdogo limetambuliwa kati ya vyombo vya habari vya ndani vya Iran na pia katika oparesheni zake nje ya nchi limeweza kuakisi habari za moja kwa moja au mubashara na kusambaza picha na video za hafla muhimu nchini Iran na eneo.
Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB ameelezea siri ya mafanikio ya Iran Press kuwa ni juhudi za kujitolea za maafisa na wafanyikazi wa shirikahilo la habari hata katika hali ngumu.