Khateebzadeh: Usalama wa Ghuba ya Uajemi ni mstari mwekundu wa Iran
-
Saeed Khateebzadeh
Msemaji wa Wizara ya Mambio ya Nchi za Nje ya Iran amesema kuwa, usalama wa eneo la Ghuba ya Uajemi ni mstari mwekundu wa Iran na kuongeza kuwa, matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu taifa la Iran si mapya bali ni kikonyo cha mnyororo wa matamshi yasiyo ya kuwajibika yanayotolewa na maafisa wa nchi hiyo dhidi ya Iran.
Saeed Khateebzadeh amewaambia waandishi wa habari mapema leo mjini Tehran kwamba, wiki iliyopita balozi mdogo wa Uinegereza na balozi wa Romania waliitwa Wizara ya Mambo ya Nje na kusailiwa kuhusiana na madai yaliyotolewa na nchi zao juu ya kushambuliwa meli katika Bahari ya Omani.
Akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu madai yaliyotolewa na maafisa wa nchi za Ulaya juu ya shambulizi lililolenga meli katika Bahari ya Oman, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu taifa la Iran si jambo jipya bali ni katika mlolongo wa matamshi yao yasiyo ya kuwajibika dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Amesema Iran pia ina wasiwasi kuhusu usalama wa safari za meli katika maji ya kimataifa na jambo hilo lilikiukwa na Uingereza miaka kadhaa iliyopita wakati uharamia wa nchi hiyo ulipofeli na hatimaye meli ya mafuta ya Iran iliyokuwa imeketwa nyara, iliachiwa huru.
Khateebzadeh amesisitiza kuwa usalama wa Ghuba ya Uajemi ni mstari mwekundu wa Iran na kwamba Tehran imefanya jitihada za kuhakikisha kwamba njia hiyo ya majini haiathiriwi na chochoko za kuvuruga amani zinazofanywa na nchi kama Uingereza. Amesema ushirikiano wa Uinegereza na utawala habithi kama Israel unaonesha vyema nafasi ya nchi hiyo mbele ya macho ya walimwengu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema Iran inatoa mkono wa pole kwa familia za wahudumu wawili wa meli hiyo waliouawa lakini inapinga njama ya kutumia tukio hilo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.