Rais Raeisi: Kustawisha uhusiano na Japan kuna umuhimu mkubwa kwa Iran
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uhusiano wa Iran na Japan ni mzuri na wa kirafiki na kwamba, kutawishwa zaidi uhusiano huo ni jambo lenye umuhimu mkubwa kwa taifa hili.
Sayyid Ibrahim Raeisi amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika mazungumzo yake na Toshimitsu Motegi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Japan na kusisitiza kwamba, Tehran ina azma ya kupanua ushirikiano wa pande zote za Tokyo hususan katika masuala ya kiuchumi na kibiashara.
Rais Ibrahim Raeisi ameeleza kuwa, kupanuliwa ushirikiano na Japan na kuweko mashirikiano mazuri zaidi baina ya pande mbili ni jambo linalopewa umuhimu mno na Jamhuri ya Kiislamu.
Sambamba na kuipongeza Japan kwa misaada yake ya kibindamu kwa ajili ya kukabiliana na Corona, Sayyid Raeisi amesema ana matumaini ushirikiano wa pande mbili utasaidia ulimwengu kung'oa kabisa mizizi ya ugonjwa huu hatari.
Kadhalika ameashiria udharura wa kuachiliwa fedha za Iran zilizozuia huko Japan na kueleza kwamba, kucheleweshwa kuachiliwa fedha hizo katika benki za nchi hiyo ni jambo lisilohalalishika.
Kwa upande wake, oshimitsu Motegi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Japan sambamba na kumpongeza Sayyid Ibrahim Raeis kwa kuanza kipindi chake cha uongozi kama Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya kupanuwa zaidi uhusiano na ushirikiano mkongwe baina ya nchi mbili hizi na kueleza bayana kwamba, mataifa haya mawili yamekuwa na uhusiano mzuri na mkongwe.