Iran yafanikiwa kuunda kifaa cha kupima vinasaba, DNA
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i73892-iran_yafanikiwa_kuunda_kifaa_cha_kupima_vinasaba_dna
Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran sasa ina teknolojia ya kujiundia kifaa cha kupima vinasaba (DNA).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 24, 2021 22:30 UTC
  • Iran yafanikiwa kuunda kifaa cha kupima vinasaba, DNA

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran sasa ina teknolojia ya kujiundia kifaa cha kupima vinasaba (DNA).

Gholam-Hussein Muhsini Ejei Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo jana Jumanne na kuongeza kuwa: "Kwa mafanikio hayo ya kuzalisha kifaa cha DNA, Iran sasa ni ya tano duniani kuwa na teknolojia hiyo baada ya Marekani, Ujerumani, China na Russia"

Ejei ameshiriki katika sherehe za kuzindua kifaa hicho cha kipimo cha vinasaba na pia kifaa kingine cha homogenizer sambamba na kutembelea Maabara ya Uchunguzi wa Vifo mjini Tehran na kusema kuna haja ya kuwaamini vijana wasomi nchini na kuwaandalia mazingira mazuri ya kufanya kazi.

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema mafanikio katika uga wa sayansi ni muhimu na dharura ili nchi iweze kufikia malengo yake ya ustawi.