Rais Raisi: Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni wa utakatifu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i74900-rais_raisi_mfumo_wa_jamhuri_ya_kiislamu_ni_wa_utakatifu
Rais Ebrahim Raisi amesema: "mfumo wetu ni wa utakatifu kwa sababu umetokana na dini na mafunzo ya dini."
(last modified 2026-08-08T07:03:00+00:00 )
Sep 21, 2021 03:45 UTC
  • Rais Raisi: Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni wa utakatifu

Rais Ebrahim Raisi amesema: "mfumo wetu ni wa utakatifu kwa sababu umetokana na dini na mafunzo ya dini."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo katika hafla ya kuadhimisha Wiki ya Kujihami Kutakatifu na kuzienzi familia za mashahidi, majeruhi wa vita na waliojitolea mhanga, ambapo sambamba na kutoa mkono wa pole kwa mnasaba wa masiku ya maombolezo ya Imam Hussein AS amebainisha kuwa: "harakati hii ya kuwakirimu na kuwenzi maveterani inaweza kukikinga kizazi cha vijana; na njia ya kukilinda kizazi cha sasa na vizazi vijavyo ni kwamba Ashura itambulishwe na ifahamike kuwa ni kitu cha mwendelezo; na mwendelezo wa leo na hivi sasa wa Ashura ni dhihirisho la mashahidi waliojitokeza kwenye medani kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya jambo takatifu.

Rais Ebrahim Raisi

Seyyid Ebrahim Raisi amesema kwa kuhoji: "Watu wengi wanapambana na kupigana vita duniani; katika muda wote wa historia vimepiganwa vita vingi na kutokea umwagikaji damu, lakini ni vipi kati ya hivyo vinaitwa "Kujihami Kutakatifu"?. Ameongezea kwa kusema: leo hii kuna mifumo mingi duniani, lakini ni upi kati ya mifumo hiyo ni mfumo mtakatifu?

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: siri ya utakatifu wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa kwake umetokana na dini, mafunzo ya dini, Kitabu cha Qur'ani na Sunna.../