Amir-Abdollahian: Jamhuri ya Kiislamu inataka kutekelezwa mapatano ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i77732-amir_abdollahian_jamhuri_ya_kiislamu_inataka_kutekelezwa_mapatano_ya_jcpoa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Syria kwamba, Iran haitaki lolote katika mazungumzo ya Vienna ghairi ya kutekelezwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 06, 2021 23:21 UTC
  • Amir-Abdollahian: Jamhuri ya Kiislamu inataka kutekelezwa mapatano ya JCPOA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Syria kwamba, Iran haitaki lolote katika mazungumzo ya Vienna ghairi ya kutekelezwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Hossein Amir-Abdollahian amesema kuwa, yaliyowasilishwa na ujumbe wa Iran kwa pande husika kama rasimu ya maandishi ni katika fremu ya mapatano ya JCPOA na kwamba Iran haijataka chochote zaidi ya yale yaliyokubaliwa na pande mbili. 

Mapatano ya nyuklia ya JCPOA 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, uhusiano wa Tehran na Damascus ni wa kistratejia na mzuri na amepongeza kujitolea, ukakamavu na wale waliouliwa shaidi kwa ajili ya kuilinda nchi na Haramu takatifu za Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) huko Iraq na Syria. Hossein Amir-Abdollahian ameongeza kuwa: "Tunawaenzi mashahidi wa Iran waliokuwa  bega kwa bega na vkosi vya ulinzi vya Syria ambao wametoa mchango mkubwa katika vita dhidi ya ugaidi na kurejesha usalama khususan Kamanda Luteni Jenerali Qasem Soleimani ambaye ametoa mchango mkubwa katika eneo Magharibi mwa Asia." 

Kuhusu mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala ghasibu wa Israel huko Syria, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Utawala bandia na wa kigaidi wa Israel ni chanzo na sababu ya kukosekama amani katika eneo la Magharibi mwa Asia na hakuna shaka kuwa Syria haijarudi nyuma na itakuwa mstari wa mbele wa muqawama na mapambano ya kulinda usalama wa taifa na ardhi ya nchi hiyo.