Kongamano la kumuenzi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes lafanyika Tunisia
(last modified Thu, 30 Dec 2021 08:17:13 GMT )
Dec 30, 2021 08:17 UTC
  • Kongamano la kumuenzi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes lafanyika Tunisia

Kundi la vyama vya siasa na asasi za kiraia nchini Tunisia zimefanya kongamano kwa mnasaba wa mwaka wa pili wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi.

Kongamano hilo lililokuwa na anuani ya 'Viongozi Mashahidi wa Muqawama Dhidi ya hujuma ya Kizayuni na Ugaidi wa Kimarekani limewakutanisha pamoja wanafikra wa Tunisia na viongozi wa jumuiya na asasi mbalimbali za kiraia.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, kufanyika kongamano hilo ni ishara kwamba, viongozi hao mashahidi wa muqawama wana nafasi katika nyoyo za washiriki wa kongamano hilo hilo nchini Tunisia.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. 

 

Hivi karibuni Rais Nicholas Maduro wa Venezuela alisema kuuwa, jamii ya kimataifa inapaswa kulaani vikali mauaji ya kigaidi ya mwaka 2020 ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani wa Iran ambaye alikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi.