Brigedia Jenerali Naserzadeh: Kamanda Soleimani ni fahari ya Ulimwengu wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i78698-brigedia_jenerali_naserzadeh_kamanda_soleimani_ni_fahari_ya_ulimwengu_wa_kiislamu
Kaimu Kamanda Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amesema, historia haitosahau hatua za thamani kubwa za kamanda Qassem Soleimani; na akaongeza kwamba, shahidi Soleimani ni fahari kwa Ulimwengu wa Kiislamu.
(last modified 2026-08-08T07:03:00+00:00 )
Jan 01, 2022 04:45 UTC
  • Brigedia Jenerali Naserzadeh: Kamanda Soleimani ni fahari ya Ulimwengu wa Kiislamu

Kaimu Kamanda Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amesema, historia haitosahau hatua za thamani kubwa za kamanda Qassem Soleimani; na akaongeza kwamba, shahidi Soleimani ni fahari kwa Ulimwengu wa Kiislamu.

Brigedia Jenerali Aziz Naserzadeh ametaja sifa za shakhsia ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani na kueleza kwamba, kutokana na shakhsia ya shahidi huyo ilivyokuwa tunaweza kusema, kamanda Soleimani ni fahari kwa Iran na mataifa yote yaliyokomboka kifikra duniani; kwa sababu huduma alizotoa kamanda Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni za kutaamali na kuzingatiwa mno katika Ulimwengu wa Kiislamu kwa kuwa zililenga kuunganisha makundi ya muqawama katika safu moja za kukabiliana na Uistikbari na Uzayuni duniani.

Naserzadeh amebainisha kuwa, kamanda Soleimani alikuwa mtu wa matendo, na kwamba unyenyekevu, ushupavu, ikhlasi na busara za shahidi huyo katika medani ya siasa na masuala ya kijeshi zilikuwa miongoni mwa sifa maalumu ambazo zimemfanya abaki ndani ya nyoyo za watu milele.

Brigedia Jenerali Aziz Naserzadeh

Kaimu Kamanda Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amesema, historia haitosahau hatua za thamani kubwa za kamanda Qassem Soleimani kwa sababu shahidi huyo alikuwa chemchemi ya huduma zenye thamani kubwa na khalisa kwa Ulimwengu wa Kiislamu; na hatua alizochukua na harakati zenye thamani alizofanya zitaendelea kubaki katika historia ya Ulimwengu wa Kiislamu na kumbukumbu za taifa la Iran.

Shahidi Soleimani ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq la al Hashdu-Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kikatili la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.../