Rais Raisi: Trump mtendajinai lazima ashtakiwe na ahukumiwe kuuawa kwa kisasi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i78790-rais_raisi_trump_mtendajinai_lazima_ashtakiwe_na_ahukumiwe_kuuawa_kwa_kisasi
Rais Ebrahim Raisi amesema, aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump ni muuaji na mhalifu mkuu wa mauaji ya kamanda Qassem Suleimani, kwa hivyo inapasa ashtakiwe na kuhukumiwa kuuawa kwa kisasi.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jan 03, 2022 11:18 UTC
  • Rais Raisi: Trump mtendajinai lazima ashtakiwe na ahukumiwe kuuawa kwa kisasi

Rais Ebrahim Raisi amesema, aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump ni muuaji na mhalifu mkuu wa mauaji ya kamanda Qassem Suleimani, kwa hivyo inapasa ashtakiwe na kuhukumiwa kuuawa kwa kisasi.

Akihutubia hadhara ya wananchi katika uwanja wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu alipouawa shahidi Al Haj Qassem Soleimani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameihutubu Marekani na maadui wengine wa taifa la Iran: "nyinyi mlidhani tarehe 13 Dei (Januari 3) ndio siku ya mwisho ya Al Haj Qassem, lakini imethibiti hiyo ni dhana batili, kwa sababu tarehe 13 Dei imekuwa siku ya kuzaliwa upya Al Haj Qassem."

Seyyid Ebrahim Raisi ameongeza kuwa, Al Haj Qassem Soleimani alikuwa mgeni rasmi wa waziri mkuu wa Iraq lakini Wamarekani waliivunja heshima ya Iraq na wakaliua taifa zima.

Rais Raisi akihutubia hadhara ya wananchi

Rais wa Iran amesema, "ikiwa utafanyika utaratibu wa kutayarisha mazingira ya kupandishwa kizimbani na kushtakiwa kiuadilifu Trump, Pompeo na wahalifu wengine katika mahakama ya haki; na jinai ya kutisha waliyofanya ikachunguzwa na wakapewa adhabu kwa matendo maovu waliyofanya, litakuwa jambo zuri sana; lakini lisipofanyika hilo, msiwe na shaka kuwa mkono wa kisasi wa umma utafanya kazi yake."

Rais Raisi amesema, kutokana na utambuzi aliokuwa nao na kwa kuelewa namna ya kuutumia uwezo na fursa, shahidi Qassem Soleimani aliibadilisha harakati ya Hizbullah ya Lebanon kuwa kambi ya muqawama kikanda na kimataifa na akaongezea kwa kusema: kutokana na Al Haj Qassem kuufahamu uwezo wa vijana, aliwaandaa na kuwaweka tayari kukabiliana na wimbi la Uistikbari kwa ari, ujasiri na ushujaa.

Kamanda mcheshi na mpenda watu, Shahidi Qassem Soleimani (kulia)

Seyyid Ebrahim Raisi amesisitiza kuwa shahidi Qassem Soleimani alikuwa Chuo cha Fikra na akabainisha kwamba: "chuo hiki cha fikra hakiwezi kufutwa kwa kombora; chuo cha fikra cha Al Haj Qassem kitabaki na kudumu.../