Shamkhani: Sauti ya kuvunja mifupa ya Uzayuni imeanza kusikika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i83092-shamkhani_sauti_ya_kuvunja_mifupa_ya_uzayuni_imeanza_kusikika
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema: "Sauti ya kuvunjwa mifupa ya Uzayuni inasikika zaidi na zaidi kimataifa."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 30, 2022 04:20 UTC
  • Shamkhani: Sauti ya kuvunja mifupa ya Uzayuni imeanza kusikika

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema: "Sauti ya kuvunjwa mifupa ya Uzayuni inasikika zaidi na zaidi kimataifa."

Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran Jumamosi leo ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter akiashiria maandamano ya Ijumaa ya jana ya Siku ya Kimataifa ya Quds Quds katika pembe mbalimbali za dunia na kusema: "Wito wa Imam Ruhullah Khomeini wa kupigania uhuru na kupambana na dhulma umekuwa na taathira kubwa zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote na umewahamasisha zaidi wapenda Mapinduzi ya Kiislamu."

Mamilioni ya watu walishiriki kwenye maandamano ya jana kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds iliyotangazwa na hayati Imam Khomeini miaka 43 iliyopita. Siku hiyo huadhimishwa katika Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuonesha mshikamano na uungaji mkono kwa mapambano ya ukombozi ya watu wa Palestina. 

Ali Shamkhani

Katika ujumbe wake wa jana kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliashiria jinai za kila aina zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni na kuongeza kuwa: Wanaodai kutetea haki za binadamu wa Ulaya na Marekani ambao walizusha makelele mengi kuhusiana na kadhia ya Ukraine, wamenyamaza kimya mbele ya jinai zinazofanyika huko Palestina na wala hawawatetei watu wanaodhulumiwa, bali kinyume chake wanamsaidia mbwa mwitu mwenye kiu ya damu. 

Ayatullah Khamenei amelitaja somo kubwa la mwenendo huo wa udanganyifu wa madola ya kibaguzi ya Magharibi kuwa ni kuepuka kuyategemea madola hayo na kuongeza kuwa: Matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu, na zaidi ya yote, suala la Palestina, hayaweza kutatuliwa isipokuwa kwa nguvu ya muqawama na mapambano inayotokana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu na sheria za Uislamu.