"Wananchi wa Palestina wako tayari kuuhami kikamilifu Msikiti wa al Aqsa"
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i83296-wananchi_wa_palestina_wako_tayari_kuuhami_kikamilifu_msikiti_wa_al_aqsa
Sekretarieti ya Mkutano wa Kimataifa wa Kuunga mkono Intifadha ya Palestina katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) imetoa taarifa na kulaani uvamizi wa Wazayuni katika Msikiti Mtukufu wa al Aqsa na kusisitiza kuwa, makundi ya muqawama na wananchi wa Palestina wako tayari kuulinda Msikiti wa al Aqsa na kuzikomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 05, 2022 22:05 UTC

Sekretarieti ya Mkutano wa Kimataifa wa Kuunga mkono Intifadha ya Palestina katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) imetoa taarifa na kulaani uvamizi wa Wazayuni katika Msikiti Mtukufu wa al Aqsa na kusisitiza kuwa, makundi ya muqawama na wananchi wa Palestina wako tayari kuulinda Msikiti wa al Aqsa na kuzikomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.

Magenge ya walowezi wa Kizayuni yaliwatolea wito Wazayuni jana Alkhamisi kuuvamia Msikiti wa al Aqsa.  Utawala wa Kizayuni wa Israel pia umelifungua lango la Al Aqsa lijulikanalo kama Bab al Magharibah na kuliruhusu kundi la kwanza la walowezi wa Kizayuni  kuingia katika eneo hilo takatifu la Waislamu. Sekretarieti ya Mkutano wa Kimataifa wa Kuunga mkono Intifadha ya Palestina ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran jana Alhamisi ilitoa taarifa na kulaani uvamizi huo wa Wazayuni katika Msikiti wa al Aqsa. 

Taarifa ya sekretarieti hiyo imeongeza kuwa, hii leo hali ya mambo imezidi kuwa mbaya katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Hali hiyo inazidisha jukumu kwa nchi zote na wapigania ukombozi kote duniani kulaani vikali njama hizi mbovu za Wazayuni dhidi ya Matukufu ya Kiislamu na ya Kikristo; zinazoendeshwa chini ya kivuli cha kimya na upuuzaji wa taasisi za kimataifa na zinazojidai kulinda haki za binadamu huku baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu wakiwasaliti na kuwafanyia khiyana waziwazi Wapalestina.  

Uvamizi wa wanajeshi wa Kizayuni katika Msikiti wa al Aqsa

Taarifa ya Sekretarieti ya Mkutano wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Intifadha ya Palestina katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran imeongeza kuwa: Uzayuni wa kimataifa na serikali ya mrengo wa kulia ya Wazayuni wenye misimamo mikali inafanya kila iwezalo ili kufuta jina la Palestina na utambulisho wa Wapalestina katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu. 

Taarifa hiyo aidha imeeleza kuwa: Wazayuni hawapaswi kujidanganya kuwa chini ya kivuli cha kuanzisha uhusiano wa kawaida na baadhi ya nchi za Kiarabu wataweza kughusubu na kupora haki halali za raia wa Palestina na mataifa ya Kiislamu na za Wakristo huko Quds na katika Msikiti wa al Aqsa. 

Duru za Palestina huko Baytul Muqaddas jana Alkhamisi zilitangaza kuwa, wanajeshi ghasibu wa Kizayuni waliwazingira na kuwashambulia Waislamu wa Palestina na walinzi wa  Msikiti wa al Aqsa; na kisha kuwafyatulia risasi.  Wapalestina kadhaa wamejeruhiwa katika ufyatuaji risasi huo wa Wazayuni.