Qalibaf: Iran imelenga katika biashara ya dola bilioni 200 na majirani zake
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i85788-qalibaf_iran_imelenga_katika_biashara_ya_dola_bilioni_200_na_majirani_zake
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran imelenga kufanya biashara ya thamani ya dola bilioni 200 na nchi jirani zake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 13, 2022 03:01 UTC
  • Qalibaf: Iran imelenga katika biashara ya dola bilioni 200 na majirani zake

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran imelenga kufanya biashara ya thamani ya dola bilioni 200 na nchi jirani zake.

Muhammad Bagheri Qalibaf leo Jumatano amekutana mjini Tashkent na kuzungumza na wafanya biashara na wazalishaji wa Kiirani wanaoishi nchini Uzbekistan na kusisitiza kuwa katika sera zake za nje Iran inatoa kipaumbele katika suala la kuzidisha mabadilishano ya kibiashara na nchi za eneo na majirani zake.  Amesema jambo hili limetiliwa mkazo pia na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Ameongeza kuwa, suala hilo litabainishwa katika hati za utekelezaji wa miradi.  

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran aidha amesisitiza namna sekta binafsi ilivyo mpambanaji mkuu katika sekta ya uchumi na kueleza kuwa serikali inapasa kujua vyema nafasi yake katika kusogeza mbele sekta ya kiuchumi katika suala la uwezeshaji, utungaji sera na kuandaa mazingira ya kufanya kazi sekta binafsi.  

Muhammad Qalibaf ameeleza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo mkubwa katika sekta ya huduma za kiuhandisi na kwa upande wa weledi; na kwa kuzingatia suhula na uwezo mkubwa uliopo kwa upande wa kasi, umakini na ubora Iran inaweza kuwa na mchango zaidi katika nyanja hizo huko Uzbekistan. 

Qalibaf jana Jumanne alielekea ziarani mjini Tashkent, Uzbekistan kwa lengo la kukutana na kushauriana na viongozi wa nchi hiyo. Kufanya mazungumzo na maspika wa mabunge ya Uzbekistan, kukuktana na wafanya biashara mbalimbali, kutembelea baadhi ya maeneo ya kitamaduni na kuimarisha kiwango cha uhusiano wa kibunge na kiuchumi kati ya nchi mbili ni kati ya malengo ya ziara ya Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Iran na ujumbe alioambatana nao katika ziara nchini Uzbekistan. 

Muhammad Qalibaf alipoelekea ziarani Uzbekistan