Kan'ani: Biden anapayukapayuka ili kuiridhisha Tel Aviv
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i86014-kan'ani_biden_anapayukapayuka_ili_kuiridhisha_tel_aviv
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa Rais wa Marekani, Joe Biden, anapayukapayuka akitoa madai kwamba Iran inataka kumiliki makombora ya nyuklia ili kuuridhisha utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 18, 2022 06:38 UTC
  • Joe Biden
    Joe Biden

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa Rais wa Marekani, Joe Biden, anapayukapayuka akitoa madai kwamba Iran inataka kumiliki makombora ya nyuklia ili kuuridhisha utawala wa Kizayuni wa Israel.

Rais wa Marekani, Joe Biden, alisema Jumamosi iliyopita kuwa nchi hiyo itaendeleza juhudi zake za kidiplomasia kuweka shinikizo kwa mpango wa nyuklia wa Iran, akisema kuwa Marekani haitairuhusu Iran kupata silaha za nyuklia.

Akijibu matamshi hayo yasiyo na msingi ya Biden, Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter leo (Jumatatu) kwamba: "Komedi ya zama zetu; Katika kipindi hiki cha kumbukumbu ya jaribio la kwanza la bomu la nyuklia la Marekani na baada ya kutembelea utawala unaokiuka sheria na unaomiliki silaha za siri za nyuklia, Biden anasisitiza kwamba "hataruhusu" Iran kutengeneza bomu la nyuklia."

Kan'ani ameongeza kuwa: Komedi hii inachezwa kwa ajili ya kuuridhisha utawala wa kibaguzi wa Israel kwa madai ya mabomu ambayo Iran haijawahi kutaka kuwa nayo.

Wakati wa safari yake ya karibuni huko Israel, Biden na waziri mkuu wa utawala huo haramu, Yair Rapid, walitoa taarifa iliyoeleza kuwa, Washington bado ina dhamira ya dhati ya kulinda usalama wa utawala wa Israel na kuhakikisha kwamba utawala huo unakua na nguvu kubwa zaidi za kijeshi katika eneo la Magharibi mwa Asia. Vilevile imesisitiza kuwa Washington haitairuhusu Iran kupata silaha za nyuklia, na kwamba Marekani iko tayari kutumia uwezo wake wa kitaifa kuhakikisha suala hilo.

Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Mahusiano ya Kigeni la Iran amesema: Iwapo vituo nyeti vya Iran vitashambuliwa Tehran italenga ndani kabisa ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kamal Kharrazi

Kamal Kharrazi ameongeza kuwa: Shambulio lolote dhidi ya usalama wa Iran kutoka nchi jirani litakabiliwa na jibu kali la Iran kwa nchi hizo, na jibu la moja kwa moja kwa utawala wa Kizayuni.