Wizara ya Upelelezi ya Iran yamnasa jasusi raia wa Sweden
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i86448-wizara_ya_upelelezi_ya_iran_yamnasa_jasusi_raia_wa_sweden
Maafisa wa Wizara ya Upelelezi ya Iran wamemtia nguvuni raia wa Sweden kwa kuhuma za kufanya ujasusi hapa nchini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 30, 2022 06:11 UTC
  • Wizara ya Upelelezi ya Iran yamnasa jasusi raia wa Sweden

Maafisa wa Wizara ya Upelelezi ya Iran wamemtia nguvuni raia wa Sweden kwa kuhuma za kufanya ujasusi hapa nchini.

Mtuhumiwa huyo wa Uswidi, ambaye alikuwa kwenye orodha ya washukiwa wa kitengo cha kupambana na ujasusi cha Wizara ya Uelelezi kutokana na mienendo na mawasiliano yake ya kutiliwa shaka katika safari zake nyingi za hapo awali nchini Iran, alikuwa chini ya uangalizi mkali wa mawakala mahiri wa kupambana na jasusi wa Wizara ya Upelelezi.

Taarifa ya Wizara ya Upelelezi ya Iran imesema kuwa: Mtuhumiwa huyo raia wa Uswidi aliingia tena nchini miezi michache iliyopita baada ya kukamatwa jasusi mwingine wa Ulaya, kwa lengo la kupata taarifa za jinsi ya kufichuka utambulisho wa jasusi huyo na aina na kiasi cha habari na taarifa za kijasusi ambazo zimenaswa na wataalamu wa Wizara ya Upelelezi ya Iran.

Mshukiwa huyo wa Kiswidi aliyekamatwa ana historia ya kusafiri katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel kabla ya kuingia nchini Iran.

Taarifa ya Wizara ya Upelelezi ya Iran imeonya kuwa, utawala wenye historia mbaya wa Sweden, ambao umewaunga mkono na kuwasaidia majasusi kadhaa wa utawala haramu wa Israel unaoikalia Quds kwa mabavu, ambao pia umekuwa makimbilio salama ya magaidi wahalifu kama wanachama wa kundi la MKO na wauaji wa wananchi na watoto wasio na hatia katika gwaride la Ahvaz, utapata jibu mwafaka iwapo utaendelea kufanya ujasusi kwa niaba na kuwaunga mkono wauaji na watendajinai.