Iran yapongeza na kuunga mkono kurefushwa usitishaji vita nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i86632-iran_yapongeza_na_kuunga_mkono_kurefushwa_usitishaji_vita_nchini_yemen
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen amefanya mazungumzo na mshauri wa ngazi za juu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambapo Tehran imesema kuwa imefurahishwa na hatua ya kurefushwa muda wa usitishaji vita nchini Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 04, 2022 02:41 UTC
  • Juhudi za Kimataifa za kutatua mgogoro wa Yemen
    Juhudi za Kimataifa za kutatua mgogoro wa Yemen

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen amefanya mazungumzo na mshauri wa ngazi za juu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambapo Tehran imesema kuwa imefurahishwa na hatua ya kurefushwa muda wa usitishaji vita nchini Yemen.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, Ali Asghar Haji amesema hayo katika mazungumzo yake na Hans Grundberg, mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendeleza juhudi zake za kuhakikisha amani ya kudumu na ya kiuadilifu inapatikana nchini Yemen. 

Pia amesema, Tehran inaamni kwamba fursa ya miezi miwili ya kurefushwa usitishaji vita itatumiwa ipasavyo kuleta maafikiano makubwa, ya kudumu na ya pande zote huko Yemen na hatimaye kuondolewa vikwazo vyote vya kiuchumi, kulipwa mishahra ya wafanyakazi, uhuru wa kutembea sehemu yoyote ya Yemen na kuanza kufanya kazi kamati za kijeshi, kiuchumi na kisisa kwa ajili ya kuhakikisha makubaliano yote yanaheshimiwa kikamilifu.

Hans Grundberg

 

Kwa upande wake, Hans Grundberg, mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen amegusia mapendekezo yaliyotolewa na umoja huo kwa pande za Yemen hivi karibuni na kutilia mkazo wajibu wa kutumiwa vizuri fursa ya usimamishaji vita, kutafuta njia za maana na za kimantiki za kuivua kikamilifu Yemen kwenye mgogoro wake wa hivi sasa. 

Pande hasimu nchini Yemen zimerefusha kwa miezi miwili makubaliano ya kusimamisha vita kwa pendekezo la Umoja wa Mataifa ingawa muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia umekuwa ukivunja mara kwa makubaliano hayo ya kusitisha mapigano huko Yemen.