Kan'ani: Utawala wa Israel unaoua watoto hauwezi kuzuia kuporomoka kwake
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i86830-kan'ani_utawala_wa_israel_unaoua_watoto_hauwezi_kuzuia_kuporomoka_kwake
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa tamko baada ya kubainika kuwa watoto 15 waliuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na kusema: "Utawala wa Israel ambao unawaua watoto, hauwezi kuzuia kuporomoka kwake kwa kuwaua watoto."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 09, 2022 05:33 UTC
  • Kan'ani: Utawala wa Israel unaoua watoto hauwezi kuzuia kuporomoka kwake

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa tamko baada ya kubainika kuwa watoto 15 waliuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na kusema: "Utawala wa Israel ambao unawaua watoto, hauwezi kuzuia kuporomoka kwake kwa kuwaua watoto."

Siku tatu za mashambulizi ya utawala haramu wa Israel huko Gaza yamesababisha vifo vya raia Wapalestina 45 wakiwemo watoto 15 na wanawake wanne huku wengine 360 wakijeruhiwa.

Mapatano ya usitishaji vita yalitangazwa kuanzia saa tano Jumapili kwa saa za Gaza (20:30 GMT). Tangu Ijumaa, utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia Gaza kwa mabomu na kusababisha hasara kubwa katika maeneo ya raia. Jeshi la Israel linadai kuwa limekuwa likiwalenga wanachama wa Harakati ya Jihad Islami wakiwemo makamanda wakuu wa kundi hilo lakini kulingana na maafisa wa Palestina, karibu nusu ya watu 45 waliokufa shahidi katika hujuma hizo za Israel ni raia.

Baadhi ya watoto waliouawa shahidi hivi karibuni katika mashambulizi ya Israel

Katika ujumbe alioutuma katika ukurasa wake wa Twitter, Nasser Kan'ani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema hakuna shaka kuwa, ndugu za watoto waliouawa shahidi katika mustakabali wa karibu wataweza kuikomboa nchi yao kutoka katika makucha ya maghasibu makatili.

Katika kujibu jinai hizo za Wazayuni, makundi ya muqawama ya Palestina yamevurumisha mamia ya makombora katika miji inayokaliwa na walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina ambazo zimepachikwa jina la Israel hasa Tel Aviv na Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion. Utawala wa Kizayuni umejaribu kuficha hasara ambazo umepata kutokana na maroketi hayo ya Wapalestina.