Jenerali Ramezan Sharif: Leo adui hathubutu kutoa vitisho dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i87254-jenerali_ramezan_sharif_leo_adui_hathubutu_kutoa_vitisho_dhidi_ya_iran
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema, kutokana na nguvu wa uwezo vilionao vikosi vya ulinzi vya Iran, leo adui hathubutu kutoa vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 20, 2022 22:33 UTC
  • Jenerali Ramezan Sharif: Leo adui hathubutu kutoa vitisho dhidi ya Iran

Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema, kutokana na nguvu wa uwezo vilionao vikosi vya ulinzi vya Iran, leo adui hathubutu kutoa vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Mfumo wa ulinzi wa Iran umejengwa na kustawishwa kwa msingi wa kuwa na kinga ya kuhakikisha adui hathubutu kuanzisha hujuma; na kuwa na uwezo wa kijeshi, silaha za kuaminika na vikosi imara vya ulinzi ndiko kunakotoa mchango mkuu wa kupatikana kinga halisi ya kuepusha hujuma.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, Brigedia Jenerali Ramezan Sharif amesema, baada ya maadui kudhoofika na kugonga mwamba katika kukabiliana na ngome imara na madhubuti ya IRGC na vikosi vingine vya ulinzi vya Iran, wameishia kupiga makelele tu ya uzushi na propaganda dhidi ya jeshi hilo la umma na la kimapinduzi la Walinzi wa Jamhuri ya Kiislamu.

 

Jenerali Ramezan Sharif ameongezea kusema, maadui wa Mapinduzi na Mfumo wa Kiislamu wanakiri kuwa wameshatumia kila wenzo uliowezekana kwa ajili ya kuliwekea mashinikizo taifa la Iran, lakini hawajafanikiwa kupata yale waliyotarajia.

Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameashiria kuzuiliwa meli ya mafuta ya Iran nchini Ugiriki, hatua iliyofuatiwa na kukamatwa meli mbili za mafuta za Ugiriki hapa nchini na akasema, kadhia hiyo ni kielelezo cha wazi cha uwezo na nguvu; na kwamba Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Sepah, linahifadhi na linalinda kwa nguvu na uwezo kamili maslahi ya taifa na malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu.../