Ebrahim Raisi: Adui amepata pigo kutokana na ustawi na maendeleo ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i89104-ebrahim_raisi_adui_amepata_pigo_kutokana_na_ustawi_na_maendeleo_ya_iran
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria ustawi wa kiuchumi iliopata Iran hivi karibuni na kusema kuwa, adui amepata pigo kutokana na jitihada na kazi kubwa inayoendelea kufanyika humu nchini kwa ajili ya ustawi na maendeleo na ndio maana anafanya kila awezalo kuhakikisha anakwamisha jitihada hizo.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Oct 09, 2022 23:20 UTC
  • Ebrahim Raisi: Adui amepata pigo kutokana na ustawi na maendeleo ya Iran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria ustawi wa kiuchumi iliopata Iran hivi karibuni na kusema kuwa, adui amepata pigo kutokana na jitihada na kazi kubwa inayoendelea kufanyika humu nchini kwa ajili ya ustawi na maendeleo na ndio maana anafanya kila awezalo kuhakikisha anakwamisha jitihada hizo.

Rais Ebrahim Raisi alisema hayo jana jioni wakati akiongoza baraza lake la mawaziri na kusisitiza kuwa, viongozi wa Iran wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kubwa zaidi kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi, kuimarisha imani, kuongeza matumaini katika jamii na kumkatisha tamaa adui. 

Vile vile amegusia matukio ya hivi karibuni humu nchini na kusisitiza kwamba, muono wa mbali na nguvu za wananchi za kuangalia mambo katika uhalisia wake zimesaidia sana kukabiliana na njama hizo mpya za maadui.

Rais Ebrahim Raisi akiongoza Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

 

Amezungumzia pia tamthimini ya kina na iliyozingatia pande zote ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kuhusu matukio ya hivi karibuni humu nchini na kuziwajibisha mamlaka za kulinda usalama katika jamii kushirikiana na wananchi kukabiliana na yeyote anayevuruga utulivu na amani na kuandaa mazingira mazuri ya kazi, jitihada na maisha ya kawaida ya wananchi.

Amesema, kulinda haki za watu ndiyo dhati na msingi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa, tukio lolote lile lazima lifuatiliwe kwa kina na kwa busara ya hali ya juu ili asije akadhulumiwa mtu yeyote lakini si sahihi kushughulishwa na masuala madogo madogo na kusahau masuala makubwa na ya kimsingi.

Kabla ya kusema hayo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa baraka na fanaka kwa Waislamu wote duniani na kwa kila mpenda haki kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Umoja inayoadhimishwa baina ya mwezi 12 na 17 Mfunguo Sita, kukumbuka siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad SAW.