Iran: Mkutano wa usalama wa Munich umepoteza hadhi yake
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i94270-iran_mkutano_wa_usalama_wa_munich_umepoteza_hadhi_yake
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikai mkutano wa usalama wa Munich na kubainisha kwamba, hatua zilizochukuliwa na waandaaji wa mkutano huo zimetoa pigo kubwa kwa itibari na hadhi ya mkutano huo wa usalama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 20, 2023 08:25 UTC
  • Iran: Mkutano wa usalama wa Munich umepoteza hadhi yake

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikai mkutano wa usalama wa Munich na kubainisha kwamba, hatua zilizochukuliwa na waandaaji wa mkutano huo zimetoa pigo kubwa kwa itibari na hadhi ya mkutano huo wa usalama.

Nasser Kan'ani Chafi amesema hayo leo katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari na kueleza kwamba, mkutano ambao unaandaliwa kwa jina la usalama unapaswa kuandaa fursa sawa kwa mataifa yote ya dunia ili yabainishe mitazamo na tathmini zao kuhusiana na changamoto zinazohusiana na usalama wa kimataifa.

Kan'ani Chafi ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa mataifa muhimu katika kuimarisha na kuboresha amani na usalama wa eneo na ni katika nchi zenye taathira na msaada mkubwa katika kuimarisha usalama wa kimataifa.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya ran ameeleza kuwa, inasikitisha kuwa Iran imenyimwa fursa ya kubainisha mitazamo na tathmini yake kuhusiana na usalama wa kieneo na dunia kwa ujumla kutokana na kutoalikwa katika mkutano wa mara hii wa usalama wa Munich.

Mkutano wa usalama wa Munich 2023

 

Kuhusiana na madai ya utawala haramu wa Israel kwamba, Iran imeshambulia meli ya utawala huo ghasibu, afisa huyo wa ngazi za juu katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekanusha vikali madai hayo.

Katika upande mwingine, Kan;ani Chafi amejibu madai ya Rais wa Azerbaijan na kusisitiza kwa kusema: "ni bora kujiepusha na ufanyaji papara katika kuhukumu mambo, uchochezi wa kisiasa na kulifanyia jambo propaganda".

Amesema hayo akijibu madai mapya dhidi ya Iran aliyotoa Rais Elham Aliyev kufuatia tukio la hivi karibuni lililojiri katika ubalozi wa Jamhuri ya Azerbaijan mjini Tehran.