Jun 29, 2023 11:28 UTC
  • Ayatullah Khatami: Hatima ya maadui wa Iran si nyingine ghairi ya kushindwa

Imamu wa Swala ya Eidul-Adh'ha iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, hatima ya maadui na upinzani dhidi ya Iran si nyingine bali ni kushindwa na kufeli katika mipango yao.

Sayyid Ayatullah Ahmad Khatami amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Eiduul Adh'ha katika chuo Kikuu cha Tehran na kueleza kwamba, wanaolifanyia uadui taifa la Iran wanapaswa kutambua kwamba, hawana hatima nyingine isipokuwa kushindwa na kugonga ukuta.

Ayatullah Khatami ameihutubu Marekani na madola ya Ulayya yanayowaunga mkono wapinzani wa mfumo wa Kiislaamu unaotawala hapa Iran na kueleza bayana kwamba, hatima ya wapinzani ambao nyinyi mnawaunga mkono ni kushindwa.

Imamu wa Swala ya Eidul-Adh'ha mjini Tehran ameashiria njama za maaduui wa Iran za kuendeleza vurugu na machafuko ya mwaka jana hapa Iran na kusema wazi kwamba, mikono ya munafikina ilianzisha machafuko mwaka jana na wakashindwa tena na kupelekea kufutwa katika siasa za Marekani na Ulaya.

Aidha amesema, hatua ya hivi karibuni ya polisi ya Albania dhidi ya wanachama wa kundi la Munafikina (MKO) ilikuwa kilele cha madhila dhidi ya kundi hilo.

Ayatullah Ahmad Khatami akiongoza Swala yaa Eidul Adh'ha katika Chuo Kikuu cha Tehran

 

Nchi za Ulaya ambazo zimekuwa mwenyeji wa makundi ya kigaidi na ya uasi dhidi ya Iran tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, hivi karibuni zimechukua hatua zinazoashiria kuwepo mabadiliko katika mtazamo wao kuhusu makundi hayo.

Hivi majuzi polisi wa Albania walishambulia makao makuu ya kundi la kigaidi la Munafikina katika mji wa pwani wa Durres, unaojulikana kama makao makuu ya Ashraf 3, na kuwatia mbaroni magaidi zaidi ya 70 ambapo gaidi mmoja aliuawa kwa kuwashambulia polisi.

Tags