Siasa za kiistratejia za Marekani; kuendelea miamala ya kiuhasama dhidi ya Iran
Seneta Christopher Andrew Coons mwanachama wa ngazi ya juu wa chama cha Democrat katika Seneti ya Marekani amesema kuwa Iran bado ni hatari na ni nchi ya kimapinduzi; na kwamba ingali ni hatari kuu ya kinyuklia kwa miongo ijayo.
Seneta Coons alisema hayo juzi Ijumaa kwenye kikao kilihofanyika katika Baraza la Uhusiano wa Nje la Seneti ya Marekani chini ya anuani "Kutathmini makubaliano ya nyuklia ya Iran baada ya mwaka mmoja."
Seneta huyo wa Marekani amesema kuwa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 yanayojulikana kwa jina la Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekezaji (JCPOA) hayakuwa ni wa ajili ya kubadili miamala ya Iran, bali mpango huo umezuia miradi ya nyuklia ya Iran.
Seneta huyo wa chama cha Democrat ambaye ni mmoja wa wawakilishi wa ngazi ya juu wa Kamati ya Uhusiano wa Nje katika Seneti ya Marekani na ambaye ni katika wale wanaodaiwa kuwa eti ni wa waungajimkono wa mpango wa JCPOA amekariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran na kuongeza kuwa, ili kuweza kuizuia Iran isimiliki silaha za nyuklia inabidi kuwepo na hatua endelevu za kuidhibiti miamala ya Iran; na kwamba hatua hizo hazipaswi kumhusisha Rais wa Marekani pekee yake, bali hatua hizo zinapaswa kupewa uzito na kuwa kipaumbele cha awali pia kwa Rais ajaye wa Marekani na idara za kiitelijinsia na wawakilishi wa Kongresi ya nchi hiyo kwa miaka mingi.
Marekani inafanya kila inachoweza kuiwekea Iran vikwazo na vizuizi vipya kwa kisingizio kuwa Tehran inajihusisha na vitendo vya kuvuruga amani na uchochezi nje ya matini ya mpango wa JCPOA.
Wizara ya Fedha ya Marekani mbali na kadhia ya nyuklia, imeiwekea Iran vizuizi vingine licha ya Tehran kuondolewa vikwazo.
Kundi maalumu lijulikanalo kwa jina la Financial Action in America mwaka 2008 lililiweka jina la Iran katika faharasa ya nchi ambazo eti ni hatari kuu kwa upande wa kifedha; na kuzitahadharisha pia benki mbalimbali kufanya miamala na Iran. Hapo jana duru za habari zilitangaza kuwa serikali ya Marekani zimelitoa kwa muda jina la Iran katika orodha ya nchi zinazotuhumiwa kutakatisha fedha na kuyadhamini kifedha makundi yanayodaiwa na Marekani kuwa eti ni ya kigaidi. Pamoja na hayo, Christopher Andrew Coons ametaka kuongezewa muda sheria ya vikwazo dhidi ya Iran ikiwa ni maandalizi ya kurejeshwa vikwazo hivyo.
Marekani inadai kuwa, Iran ni serikali isiyotekeleza vizuri majukumu yake. Matamshi ya seneta huyo wa Marekani pia yanadhihirisha mtazamo huo. Kuunga mkono haki za wananchi wa Palestina na Yemen na hatua ya Iran ya kuendesha vita dhidi ya makundi ya kigaidi huko Iraq na Syria; na vile vile nguvu zake za makombora ya balistiki, ndiyo mambo ambayo yanaifanya Marekani inadai kuwa Iran ni serikali isiyowajibika.
Madai hayo yote yanatolewa katika hali ambayo Iran imetekeleza vizuri makubaliano ya nyuklia ya JCPOA katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita; huku upande wa pili hususan Marekani ukishindwa kutekeleza ahadi zake. Aidha baadhi ya vikwazo dhidi ya Iran havijaondolewa huku ushirikiano kati ya Iran na mabenki mbalimbali ukiendelea kutatizwa na kuwekewa vizuri mbalimbali. Wakati huo huo viongozi wa serikali ya Marekani wanadai kuwa hakuna kizuizi chochote katika miamala ya kibenki na Iran, hata hivyo kivitendo viongozi hao wanazuia benki za dunia kufanya miamala na Iran. Ni wazi kuwa uadui na kufeli njama za Marekani hakuishii tu katika mpango wa JCPOA; bali uadui huo unashuhudiwa pia katika matamshi na misimamo ya viongozi wa serikali ya Marekani. Mtazamo huo unaonyesha wazi uhasama mkubwa wa Marekani didi ya Iran na kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, vitendo hivyo vya Marekani vinadhihirisha ukweli kuwa, asili ya Marekani haijabadilika na hakuna tofauti yoyote kati ya Wademocrat na Warepublic huko Marekani katika kukabiliana Iran.