-
Kiongozi Shahidi Ayatullah Khamenei azikwa katika Haram ya Imam Ridha (a.s) mjini Mash'had
Jul 11, 2026 02:37Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Sayyid Aali Khamenei amezikwa katika Haram ya Imam Ridha (a.s) mjini Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran.
-
Mamilioni wahudhuria mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika mji wa Mash'had
Jul 09, 2026 15:25Shughuli maalumu ya kuuaga na kuusindikiza mwili wa kiongozi shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei pamoja na mashahidi wa familia yake imefanyika leo katika mji mtakatufu wa Mash'had.
-
Iran yapeleka malalamiko ya kushambuliwa vituo vyake vya anga za mbali katika Umoja wa Mataifa
Jul 09, 2026 12:01Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali mashambulizi haramu ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya vituo vyake vya anga za mbali na kuwasilisha malalamiko yake rasmi kuhusu suala hilo katika kikao cha jopo kazi la Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mashindano ya silaha katika anga za juu, ikitoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka na jamii ya kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na matumizi ya silaha katika anga hizo.
-
Baada ya mamilioni kutoa heshima kwa Shahidi Khamenei nchini Iraq, Tehran yasema tukio hilo limetuma ujumbe wa umoja wa Umma
Jul 09, 2026 09:43Katika ujumbe uliotolewa mapema leo Alkhamisi, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Brigedia Jenerali Esmail Qaani ametoa shukrani kwa taifa na serikali ya Iraq kwa maandalizi mazuri ya mazishi ya Kiongozi aliyeuawa shahidi wa Mapinduzui ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei na watu wa familia yake.
-
IRGC yashambulia miundombinu muhimu ya Marekani huko Kuwait, Bahrain kama sehemu ya majibu ya awali
Jul 09, 2026 08:48Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limeshambulia miundombinu muhimu katika kambi nne za Marekani huko Kuwait na Bahrain katika awamu ya kwanza ya majibu yake dhidi ya ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha vita unaofanywa na Marekani.
-
Ni mabadiliko gani ya kisiasa na kiusalama yanayofuatiliwa na Marekani kwa kuendelea kukiuka makubaliano ya kusitisha vita?
Jul 09, 2026 07:07Katika saa za alfajiri ya Jumatano, Julai 8, 2026, jeshi la Marekani, kwa kukiuka waziwazi vifungu vya 2 na 4 vya Hati ya Umoja wa Mataifa na kifungu cha kwanza cha makubaliano ya kusitisha vita, limefanya mashambulizi ya kichokozi katika vituo vya ufuatiliaji na usimamzi katika pwani ya kusini mwa Iran.
-
Rais Pezeshkian: Mazishi ya Kiongozi wa Iran ni kielelezo cha umoja wa kitaifa
Jul 09, 2026 03:33Rais Masoud Pezeshkian amesema mahudhurio makubwa ya watu kutoka matabaka yote ya jamii katika mazishi makubwa yaliyofanyika kwa ajili ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ni kielelezo cha umoja wa kitaifa nchini Iran.
-
Pezeshkian: Unyanyasaji wa Marekani katika Kombe la Dunia unaakisi sera ya kigeni ya Washington
Jul 09, 2026 03:30Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema Marekani imegeuza Kombe la Dunia FIFA la 2026 kuwa uwanja mwingine wa uonevu na mashinikizo ya kisiasa, akisisitiza kuwa mwenendo wa Washington kama mwenyeji wa michezo hiyo unaonyesha sera zile zile inazotekeleza kote duniani.
-
Spika wa Bunge la Iran: Zama za uonevu wa Marekani zimekwisha
Jul 09, 2026 03:26Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ameikosoa Marekani kwa kukiuka Mkataba wa Maelewano kati ya Iran na Marekani (MoU), akisisitiza kwamba "zama za uonevu na ulaghai" wa Washington zimekwisha.
-
Mamilioni wamuaga Kiongozi Shahidi Ayatullah Khamenei katika miji ya Najaf na Karbala nchini Iraq
Jul 08, 2026 14:19Mamilioni ya waombolezaji leo Jumatano walikusanyika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala nchini Iraq kwa ajili ya kuaga na kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na familia yake waliouliwa shahidi katika mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.