-
Kwa nini sera ya Marekani ya "mashinikizo ya juu zaidi" ni marudio ya mkakati uliofeli?
Aug 25, 2026 10:17Richard Nephew, mmoja wa wabunifu wakuu wa mfumo wa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran, amekosoa mbinu ya sasa ya Washington, akisema sera ya "kuongeza mashinikizo ya kiuchumi" haina tija wala msingi mzuri wa kimkakati.
-
Rais Pezeshkian: Umoja wa kitaifa kinga ya Iran dhidi ya vitisho vya nje
Aug 25, 2026 03:24Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa kulinda umoja na mshikamano wa kitaifa, akisema kuwa kukabiliana na vitisho vya nje kunahitaji ushirikiano, kuzingatia haki na kushughulikia matatizo ya kiuchumi pamoja na changamoto za maisha zinazowakabili wananchi.
-
Mkuu wa Jeshi: Wairani wako tayari kupambana kwa vizazi 20 vijavyo, hawatakubali ardhi yao idhuriwe
Aug 25, 2026 03:16Kamanda mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anasema kuwa taifa liko tayari kupambana kwa vizazi vijavyo ili kuzuia maadui na mataifa ya kigeni kubadili sura ya nchi yao, akisisitiza kuwa Wairani hawatakubali ardhi yao ya asili idhuriwe.
-
“Umma wa Mtume” ni Kaulimbiu Kuu ya Wiki ya Umoja wa Kiislamu
Aug 25, 2026 03:14Katibu wa Makao Makuu ya Wiki ya Umoja wa Kiislamu nchini Iran ametangaza kuwa kaulimbiu kuu ya hafla ya mwaka huu ni “Ummah wa Mtume Mtukufu (SAW).”
-
Madaktari wa Iran wazindua mbinu mpya ya tiba ya saratani ‘isiyo na kifani duniani kote’
Aug 25, 2026 03:10Madaktari wa Iran wamezindua mbinu mpya ya uchunguzi na tiba ya saratani sugu na zilizosambaa mwilini (metastatic solid cancers), wakiielezea kama mbinu ya kwanza ya aina yake kuvumbuliwa na kutumiwa ulimwenguni.
-
Hakuna nchi inayopasa kutuhofia iwapo haiwasaidii wavamizi
Aug 24, 2026 13:49Iran imesema kuwa nchi hazipaswi kuwa na wasiwasi wowote kuhusu Jamhuri ya Kiislamu, isipokuwa pale zinapozipatia pande zinazotekeleza vitendo vya uhalifu na uvamizi vituo, miundombinu au zana ili kutekeleza mashambulizi dhidi yake.
-
Iran ndiyo nguvu mpya ya kikanda, si Marekani au 'Israel': The Atlantic
Aug 24, 2026 13:43Mtaalamu maarufu wa masuala ya kimikakati wa kihafidhina wa Marekani amesema kwamba vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimekuwa na matokeo kinyume na matarajio, na vimeshindwa kuilazimisha Tehran kusalimu amri, na badala yake vimeimarisha ushawishi wa Iran wa kikanda, vikifichua mipaka ya nguvu za kijeshi za Marekani na kugeuza Lango-Bahari la Hormuz kuwa chanzo kikuu cha ushawishi wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Vita vya Kiuchumi vya Trump Dhidi ya Iran: Chombo Ambacho Hakifanyi Kazi Tena
Aug 24, 2026 10:58Katika kujibu vitisho vipya vya Donald Trump dhidi ya Iran, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, "kung'ang'ania sera zilizofeli kutapelekea tu kushindwa zaidi na kuchochea chuki ya wananchi wa Iran dhidi ya watawala wa Marekani."
-
PGSA: Iran itazuilia na kutwaa meli zinazokiuka sheria za Lango-Bahari la Hormuz
Aug 24, 2026 06:15Mamlaka ya Lango-Bahari la Ghuba ya Uajemi (PGSA), ambayo ni chombo cha udhibiti cha Iran cha Lango-Bahari la Hormuz, imetangaza kwamba meli zinazokiuka itifaki za Iran za njia hiyo ya majini ya kimkakati zitakabiliwa na vikwazo kwenye njia za baadaye, ikiwa ni pamoja na faini, kuzuiliwa, au kutwaliwa.
-
Pezeshkian: Ulimwengu umeshangazwa na ustahimilivu wa Iran katika vita vya Marekani na Israel
Aug 23, 2026 14:26Rais Masoud Pezeshkian amesema kuwa tathmini ya adui kwamba Iran itasambaratika kutokana na mashinikizo makubwa haikuwa sahihi na kwamba mshikamano na umoja wa taifa hili vimeishangaza dunia.