-
Vita vya Kiuchumi vya Trump Dhidi ya Iran: Chombo Ambacho Hakifanyi Kazi Tena
Aug 24, 2026 10:58Katika kujibu vitisho vipya vya Donald Trump dhidi ya Iran, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, "kung'ang'ania sera zilizofeli kutapelekea tu kushindwa zaidi na kuchochea chuki ya wananchi wa Iran dhidi ya watawala wa Marekani."
-
PGSA: Iran itazuilia na kutwaa meli zinazokiuka sheria za Lango-Bahari la Hormuz
Aug 24, 2026 06:15Mamlaka ya Lango-Bahari la Ghuba ya Uajemi (PGSA), ambayo ni chombo cha udhibiti cha Iran cha Lango-Bahari la Hormuz, imetangaza kwamba meli zinazokiuka itifaki za Iran za njia hiyo ya majini ya kimkakati zitakabiliwa na vikwazo kwenye njia za baadaye, ikiwa ni pamoja na faini, kuzuiliwa, au kutwaliwa.
-
Pezeshkian: Ulimwengu umeshangazwa na ustahimilivu wa Iran katika vita vya Marekani na Israel
Aug 23, 2026 14:26Rais Masoud Pezeshkian amesema kuwa tathmini ya adui kwamba Iran itasambaratika kutokana na mashinikizo makubwa haikuwa sahihi na kwamba mshikamano na umoja wa taifa hili vimeishangaza dunia.
-
Mkuu wa Usalama: Iran itaendelea kufunga Hormuz hadi Marekani itimize majukumu yake
Aug 23, 2026 14:24Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itafubaza mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani ikiwa ni pamoja na kuzichukulia hatua nchi ambazo zinashiriki katika “vita vya kiuchumi” vya Marekani dhidi ya Iran.
-
Kaimu Waziri wa Ulinzi: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitasalimu amri kwa kuwekewa mashinikizo
Aug 23, 2026 03:28Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema, taifa hili limeishinda kimkakati Marekani na utawala wa Kizayuni kwa kutegemea uwezo wake wa ndani, na akasisitiza kwamba: Jamhuri ya Kiislamu haitasalimu amri katu kwa kuwekewa mashinikizo.
-
Meja Jenerali Safavi: Jina la Iran linapaswa kuwa jinamizi la daima kwa tawala vamizi
Aug 22, 2026 12:24Mshauri Mkuu wa Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meja Jenerali Sayyed Yahya Rahim Safavi, amesema uzoefu wa Iran katika vita na makabiliano yake na Marekani na utawala wa Israel unaonesha umuhimu wa kuimarisha uwezo wa kiulinzi na kujenga nguvu ya kuzuia uchokozi.
-
Iran yalaani vikwazo vipya vya Marekani na kuvitaja kuwa hujuma dhidi ya mamlaka ya nchi
Aug 22, 2026 12:22Iran imelaani vikali vikwazo vipya vya kiuchumi vilivyotangazwa na Marekani, ikisema hatua hiyo ni ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala nchi huru na jaribio la Washington la kujipa mamlaka juu ya mataifa mengine.
-
Salehi-Amiri: Afrika Kusini ni lango la Iran kuingia katika soko la utalii barani Afrika
Aug 22, 2026 12:20Waziri wa Urithi wa Utamaduni, Utalii na Kazi za Mikono wa Iran, Seyyed Reza Salehi-Amiri, amesema Afrika Kusini inaweza kuwa lango la Iran kuingia katika soko la utalii barani Afrika, akisisitiza umuhimu wa kubadilisha mazungumzo ya kisiasa na kidiplomasia kuwa ushirikiano wa kivitendo na wa kiuchumi.
-
Iran yaendelea kuboresha sekta yake ya ulinzi baada ya vita vya Marekani na Israel
Aug 22, 2026 02:55Wizara ya Ulinzi ya Iran imesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu inaendelea kuifanya sekta yake ya ulinzi kuwa ya kisasa, ikizingatia mahitaji yaliyojitokeza kutokana na vita vya hivi karibuni vilivyolazimishwa dhidi ya nchi hii na Marekani na Israel.
-
Iran: Vikwazo vipya vya Marekani ni ‘ugaidi wa kiuchumi’ na ‘uhalifu dhidi ya ubinadamu’
Aug 21, 2026 10:34Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali mzunguko mpya wa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hili, ikisisitiza kuwa hatua hizo ni sawa na “ugaidi wa kiuchumi” na “uhalifu dhidi ya ubinadamu.”